Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latiffa Mohammed, akizungumza
na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani), kuhusu Mafanikio ya TANTRADE
kwa maiaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano uliofanyika
Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latiffa Mohammed, akizungumza
na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani), kuhusu Mafanikio ya TANTRADE
kwa maiaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano uliofanyika
Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.
……………..
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TANTRADE) katika kipindi cha miaka
minne ya Uongozi wa
Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kuziunganisha kampuni 31,891
kuweza kupata taarifa za bei na masoko ya bidhaa za ndani na nje ya
nchi.
Hayo yamebainishwa leo Jumatano
(Novemba 27, 2019) Jijini Dar es Salaam na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
TANTRADE, Latifa Khamis wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya
Taasisi hiyo katika Kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Serikali ya
Awamu ya Tano kuanzia Novemba 2015 hadi Novemba 2019.
Alisema kuwa ya wafanyabiashara
hao, TANTRADE iliweza kuunganisha katika masoko wafanyabiashara 405 na
kuuza tani 102,000 za mahindi, tani 2,000 za karanga, tani 5,000 za
soya, tani 50 za ufuta, tani 7 za majani ya papai, kilogramu 200 za unga
wa ubuyu, tani 2 za iliki, tani 5,000 za muhogo na tani 3.2 za
tangawizi ya unga.
Aliongeza kuwa miongoni mwa bidhaa
zilizoonesha uhitaji mkubwa katika masoko ya nje ni pamoja na matunda,
samaki na mazao ya bahari, jamii ya mikunde, asali, kahawa, chai,
korosho, viungo na vyakula, ambapo maulizo ya bidhaa hizo yalitoka
katika nchi za India, Nchi za Kiarabu, Misri, Marekani, Vietnam na
Ulaya.
‘’Mbali na kusambaza taarifa za
uhitaji wa bidhaa mbalimbali TANTRADE kwa kushirikiana na wanunuzi
kutoka nchi zao tumewezesha kupatikana kwa muendelezo wa kimkakati wa
kupenya katika masoko yao, semina mbalimbali ziliratibiwa ambapo
wafanyabiashara na wadau 425 walishiriki ili kutambua fursa za masoko ya
nje na taratibu za kuyafikia’’ alisema Latifa.
Kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa
masoko ya nje ya nchi, Latifa alisema TANTRADE imeendelea kuratibu
maonesho ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) kwa lengo la
kutoa fursa za kutangaza bidhaa zilizoongezewa thamani na upatikanaji wa
teknolojia ili kupanua wigo wa masoko ya nje ya nchi.
Latifa alisema kupitia DITF kila
mwaka Tanzania hupokea wastani wa kampuni 500 kutoka zaidi ya nchi 35
zinazoshiriki maonesho hayo na hivyo kuwasaidia wafanyabiashara katika
upatikanaji wa teknolojia na kusaidia kutatua changamoto za uzalishaji
hafifu wa bidhaa za kilimo, uchenjuaji wa madini na hivyo kuleta matokeo
chanya yaliyokusudiwa.
Akifafanua zaidi Latifa alisema
kwa mwaka 2019 pekee kupitia DITF, mafanikio mbalimbali yaliweza
kupatikana ikiwemo kampuni 437 kupata oda ya kufanya biashara zenye
thamani ya Tsh Bilioni 7.93, kufanyika kwa mauzo ya papo kwa papo yenye
thamani ya wastani wa Tsh. Milioni 209, pamoja na kutengeneza ajira za
muda mfupi zipatazo 14,912 zilizotokana na kazi mbalimbali za maonesho
ikiwemo ujenzi, ulinzi na usafi.
Akizungumzia kuhusu ushiriki wa
Tanzania katika maonesho ya nje ya nchi, Latifa alisema Tanzania
imefanikiwa kushiriki katika maonesho katika nchi zilizo na utengamano
ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi
za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo wastani wa kampuni 200 zimeweza
kushiriki na kutambua bidhaa zao kwenye nchi hizo na kuingia mikataba ya
kibiashara ili kupata masoko endelevu.
Akitoa mfano Latifa alisema katika
mwaka 2018/19, Tanzania ilishiriki maonesho ya 15 ya Biashara China
ambapo kampuni 20 zilishiriki na kuweza kutafutiwa masoko ya bidhaa na
kutangaza vivutio mbalimbali vya uwekezaji ikiwemo vivutio vya utalii,
mazao ya kilimo hususani kahawa, chai, karafuu, asali, korosho, mazao ya
jamii ya kunde na bidhaa za mikono ikiwemo vikoi.
‘’Katika maonesho ya chakula ya
Gulfood-Dubai kampuni tatu zaTanzania zilifanikiwa kutembelea maonesho
hayo yaliyofanyika Dubai kwa lengo la kutambua fursa mbalimbali kutoka
kwa washiriki, ambapo wanunuzi wa bidhaa mbalimbali kama asali kontena
30, kahawa tani 50, ukwaju tani 10 walipatikana’’ alisema Latifa.
Aidha Latifa alisema TANTRADE
katika kutekeleza adhima ya Tanzania ya Viwanda ilianzisha maonesho ya
bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika kila mwezi Desemba, ambapo
tangu kuanza kwake mwaka 2007 wastani wa makampuni 497 hushiriki na
kuwafanya wazalishaji wa bidhaa nchini kupata fursa ya kutambulisha
bidhaa zao na kuhamasisha matumizi ya bidhaa za Tanzania.
No comments :
Post a Comment