
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja
na Viongozi na Wafanyakazi wa Boti mpya ya Kilimanjaro VII baada ya
kuizindua na kuitembelea iliofanyika katika Hoteli ya Verde mjini
Zanzibar.

Mmiliki wa Mradi wa Ujenzi wa Boti
Salim Azizi Salim akitoa maelezo kuhusiana na Mtengenezo ya Boti mpya
ya Kilimanjaro VII amabayo imezinduliwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya
Verde mjini Zanzibar.

Waziri wa Fedha na Mipango Baloz
Mohamed Ramia Abdiwawa akitoa hotuba ya makaribisho katika hafla ya
Uzinduzi wa Boti Mpya ya Kilimanjaro VII iliofanyika katika Hoteli ya
Verde mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akibonyeza kitufe cha
kulazia Kiti wakati alipotembelea Boti ya Kilimanjaro VII (SABA)Baada ya
kuizindua katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati akitoa
hotuba ya Uzinduzi wa Boti Mpya ya Kilimanjaro VII(SABA) hafla
iliofanyika Hoteli ya Verde Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria
Uzinduzi wa Boti mpya ya kilimanjaro VII (SABA)iliofanyika katika Hoteli
ya Verde mjini Zanzibar.kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Baloz Seif Ali Idi,mwengine ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Azam Said
Salim Bakhresa na kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi
Mohamed Ramia Abdiwawa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa
Mwenyekiti wa Makampuni ya Azam Said Salim Bakhresa kuhusiana na ubora
wa Vifaa vya ndani ya Boti mpya ya Kilimanjaro VII(SABA)ikiwemo Viti vya
kukunja na kukunjuwa baada ya kuizindua katika Hoteli ya Verde mjini
Zanzibar.
No comments :
Post a Comment