Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na waandishi wa habari
akiwaelezea mikakati ya jinsi Wizara ya Maliasili na
utalii,ilivyojipanga kushirikiana na wasanii katika kutangaza vuvitio
vya utalii katika mkutano uliofanyika jana jioni JIjini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja ya baadhi
ya Miss Tourism Tanzania waliokuwa washindi wa mashindano katika miaka
minne iliyopita

Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti Afisa wa Wanyamapori
wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAW) Mary Kagasheki
aliyewasilisha mada ya Utalii katika mkutano uliowakutanisha wasanii
mbalimbli nchini katika maandalizi ya awali ya kumtafuta miss Tourism
Tanzania.
( Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
**************************************
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewapongeza Wasanii kwa
kuonesha utayari wa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika
kunadi vivutio vya Utalii.
Kufuatia hali hiyo,
Mhe.Kanyasu amewahakikishia Wasanii hao kuwa yeye pamoja na Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangala wapo tayari muda wote kutoa
ushirikiano kwa Msanii yeyote atakayetaka kufanya kazi na Wizara hiyo.
Akizungumza na
wasanii mbalimbali pamoja na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam
jana usiku, Mhe.Kanyasu amesema kazi ya sanaa nchini inakua kwa kasi
sana, Hivyo wasanii hawawezi kuachwa nyuma katika kutangaza na
kuhamasisha Utalii
Katika Mkutano huo
uliwakutanisha Wasanii mbalimbali wakiwemo wa wasanii
filamu,vichekesho, uchongaji pamoja Washindi wa Miss Utaliu wa miaka
minne iliyopita. Mhe.Kanyasu amesema Sanaa ni kichochea cha utalii.
Amesema ushirikiano
huo wa Wasanii ni hatua muhimu kwa katika kufikia azma ya Serikali ya
awamu ya tano ifikapo mwaka 2020 ni kufikisha idadi ya watalii mbili na
nusu.
Akizungumzia
mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya nne tangu yalipoanzishwa,
Mhe.Kanyasu amewapongeza waandaaji wa Mashindano hayo kwa kubuni
vipengele viwili vya kuwatafuta Walimbwende yaani Mlimbwende Utalii wa
Tanzania pamoja na Mlimbwende wa Utalii wa Kimataifa. ( Miss Tourism
Tanzania & Miss Tourism International )
Amesema ubunifu huo
utasaidia kunadi vivutio vya utalii kitaifa kwa kumtumia Mlimbwende wa
Utalii wa Tanzania huku vivutio hivyo vya Utalii vitadiwa Kimataifa na
Mlimbwende wa Utalii wa Kimataifa.
Ameongeza kuwa mashindano hayo yana sura mpya kwa kuzingatia muono wa Kitaifa na Kimataifa.
Kwa upande wake,
Mratibu wa Mashindano hayo, Gideon Chipungahelo amesema vigezo vya
kuwapata Washindi hao mbali ya Ulimbwende watakaokuwa nao watazingatia
uelewa walionao katika kuvijua vivutio vya Utalii vilivyopo nchini
” Tunamtaka
Mlimbwende atakayekuwa balozi wa Utalii na Mwenyekiti ushawishi wa
kuwafanya watu wengine wahamasike kutembelea vivutio vya Utalii
vilivyopo nchini.” alisisitiza Mratibu huyo..
Akizungumzia
maandalizi ya Maonesho hayo, Chipungahelo amesema yataanza mwezi
Disemba na kumalizika mwezi Machi mwakani ambapo yatafanyikia jijini
Dar es Salaam .
Aidha, Mratibu huyo,
Chipungahello amesema kwa upande wa Mashindano ya Utalii wa Kimataifa,
nchi 56 zimeonesha utayari wa kushiriki katika Mashindano hayo.
Naye, Mwakilishi wa
Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA,) Anna Masenge amesema Mashindano hayo
yatazingatia maadili ya Mtanzani na kamwe hayatakuwa kichocheo cha
kuharibu utamaduni huo kwa vile Waandaji hao watazingatia kanuni na
miongozo iliyotolewa na BASATA
Kufuatia hali hiyo
ametoa wito kwa wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika
kinyang’iro hicho huku akiwatoa hofu wazazi kuwa Mashindano hayo sio
uhuni kama wengi wanavyoyachukulia.
No comments :
Post a Comment