Saturday, November 30, 2019

MH.UMMY MWALIMU AZINDUA CHUMBA CHA KUHIFADHI MAJOKOFU YA UMEME KWENYE ZAHANATI YA NYAKASUNGWA WILAYANI SENGEREMA.



***********************************
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amezindua chumba cha kuhifadhia majokofu yanayotumia umeme wa jua kwenye zahanati ya
Nyakasungwa iliyopo halmashauli ya Buchosa wilayani Sengerema.
Halmashauri ya buchosa imepata majokofu 17 kutoka Wizara ya afya mwezi oktoba 2019 kwa awamu ya kwanza na tayari yamesambazwa kwenye na kufungwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Hali ya chanjo kwa halmashauri hiyo kwa kwa mwaka huu ni asilimia 94 kutoka asilimia 79 mwaka jana na katika kampeni ya kitaifa ya chanjo ya surua na rubella mwezi oktoba mwaka huu imefanikiwa kwa asilimia 106.
Majokofu hayo yatasaidia kuimarisha mnyororo baridi na hivuo kuongeza ubora na utunzaji wa chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya ambayo itapelekea watoto kupata chanjo zenye ubora kama ilivyokusudiwa

No comments :

Post a Comment