Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais- Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akipokea wasilisho
la mpango wa fursa za uwekezaji katika bonde la Mto Msimbazi na
suluhisho la kudumu la mafuriko yanayotokea jijini Dar Es Salaam kutoka
kwa Mwakilishi wa DFID Bwana Boshell. Kikao hiko kime fanyika jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais- Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akiwa katika picha
ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mh. Suleiman Jafo
wakati wa kikao cha kupokea wasilisho la mpango wa fursa za uwekezaji
katika bonde la Mto Msimbazi na suluhisho la kudumu la mafuriko
yanayotokea jijini Dar Es Salaam.
Sehemu ya Maafisa wa Serikali
kutoka Wizara mbalimbali waliohudhuria katika kikao hiko cha kupokea
wasilisho la mpango wa fursa za uwekezaji katika bonde la Mto Msimbazi
na suluhisho la kudumu la mafuriko yanayotokea jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-
TAMISEMI Mh. Suleiman Jafo akipokea wasilisho la mpango wa fursa za
uwekezaji katika bonde la Mto Msimbazi na suluhisho la kudumu la
mafuriko yanayotokea jijini Dar Es Salaamkutoka kwa Mwakilishi wa Benki
ya Dunia Bwana Yohannes Kesete. Kikao hiko kilifanyika jijini Dar es
Salaam.
……………
Uelewa Zaidi juu ya mradi wa
ujenzi wa mto Msimbazi unatakiwa kutolewa ili mradi huo
uweze
kufanikiwa. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-
Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene alipokua akipokea
wasilisho la mpango wa fursa za uwekezaji katika bonde la Mto Msimbazi
na suluhisho la kudumu la mafuriko katika jiji la Dar es salaam. Kikao
hiko kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa TAMISEMI jijini Dar Es
Salaam.
“Mradi huu ni muhimu sana na
uchambuzi wa kina unahitajika pamoja na uelewa Zaidi ili kuweza
kukamilisha mradi huu na kila mmoja anatakiwa kuona umuhimu wa mradi
huu” alisema Waziri Simbachawene.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais-TAMISEMI Mh. Suleiman Jafo akiongea katika kikao hiko alisema kuwa
mradi huo ni fursa ya uwekezaji katika jiji la Dar es Salaam ukifanikiwa
basi mandhari ya jiji la Dar Es Salaam itapendeza na kuwa kivutio cha
utalii hivyo kulinufaisha Taifa kiuchumi.
Kikao hiko cha kupokea wasilisho
la mpango wa fursa za uwekezaji katika bonde la Mto Msimbazi
kimeandaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na
Mazingira Mh. George Simbachawene, ikiwa ni maelekezo ya Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, aliyotoa
ili kutafuta suluhu ya kudumu ya mafuriko katika jiji la Dar es Salaam
na kuondoa madhara yanayosababishwa na mafuriko.
Mawaziri wengine waliotakiwa
kushiriki katika upokeaji wa wasilisho hilo ni Waziri wa fedha na
Mipango, Waziri wa Mawasiliano, ujenzi na Uchukuzi, Waziri wa Maji na
Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ambao waliwakilishwa na
Wawakilishi kutoka Wizara zao.
No comments :
Post a Comment