Thursday, November 28, 2019

MADAI YA FIDIA KWA NJIA YA MTANDAO KUONGEZA TIJA KAZINI: DKT. OMARY


 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, akizungumza mwanzoni mwa mafunzo ya siku moja kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi kwa wanachama wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka
 Mtaalamu wa TEHAMA, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Mihayo Mathayo, ya huduma zitolewazo na Mfuko kupitia Mtandao (Self Service Portal)
 Meneja Madai Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akiwasilisha mada kuhusu Mafao yatolewayo na WCF.
Kutoka kushoto, Meneja Madai WCF, Bi. Rehema Kabongo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, Mwanasheria wa Mfuko, Bw. Deo Ngowi na Bw. Pascal Richard kutoka kitengo cha Usajili na Uwasilishaji Michango WCF, wakinakili hoja na maswali yaliyoelekezwa kwenye Mfujo na washiriki, wakati wa majadiliano.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MABORESHO makubwa ya utoaji taarifa za ajali, magonjwa na vifo vitokanavyo na kazi kwa kutumia mtandao “e-notification” yamelenga kusogeza karibu kabisa huduma za Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) kwa wadau wake na hivyo kuongeza tija, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omary amewaambia wanachama wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) wakati wa semina ya mafunzo ya siku moja iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Kwa sasa wadau wa Mfuko ambao wanatumia huduma za mtandao hawalazimiki kufika kwenye ofisi zetu ili kuhudumiwa, bali wanaweza kupata huduma hizo kutoka mahala popote na wakati wowote na tunaamini hatua hii imepunguza gharama na kuokoa  muda ambao utaongeza uzalishaji na hivyo kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.” Alisema Dkt. Omary ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba, katika ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Nchini (ATE).

Dkt. Omary alisema Mfumo huu unamwezesha Mwajiri kutoa taarifa ya tukio kwa wakati kuwasilisha nyaraka na kujua hatua iliyofikiwa katika uchakataji wa madai ya fidia kwa njia ya mtandao.

Mfuko umetoa fursa kwa wateja wake kupata huduma mbalimbali kupitia mifumo ya kielektroniki (TEHAMA), alisema.

Akiwasiklisha mada ya jihudumie kupitia mtandao (Self Service Portal) Mtaalamu wa TEHAMA, wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Mihayo Mathayo alisema Mifumo hiyo iliyosimikwa ni pamoja na Mfumo wa Usajili ambao unamuwezesha mwajiri kujisajili (e-registration) na kupata hati ya usajili papo hapo, anafafanua mtaalamu wa IT kutoka WCF, Bw. Mihayo Mathayo.

Bw. Mihayo alitaja Mifumo mingine kuwa ni pamoja na Uwasilishaji michango ambao unamwezesha Mwajiri kutnza taarifa za wafanyaakazi na kuwasilisha michango kupitia nambari ya udhibiti yaani Control Number na kupata stakabadhi ya kielektroniki.

“Jambo la kufurahisha, mteja utatumia si zaidi ya dakika tano kupata huduma ukitumia mfumo huu wa TEHAMA, na hivyo kuleta tofauti kubwa sana na hapo awali ambapo kwanza mteja analazimika kufunga safari na kuzifata ofisi za Mfuko ili kuhudumiwa na hivyo kusababisha upotevu wa muda.” Alifafanua Bw. Mihayo.

Kwa upandew wake, MKURUGENZI Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka, aliushukuru uongozi wa WCF kwa kutenga muda wao kutoa elimu hiyo muhimu kwa wanachama wake, kwani itasaidia sana katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mbali na kujifunza masuala hayo ya huduma zitolewazo na WCF kupitia Mtandao, washiriki hao pia walipatiwa mafunzo mbalimbali yakiwemo Sheria iliyoanzisha Mfuko, Kujisajili na jinsi ya kuwasilisha michango WCF na namna ya kuwasilisha madai ya Fidia na  Mafao yanayotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.

No comments :

Post a Comment