Msajili wa Baraza la Famansia
nchini, Elizabeth Shekalaghe akizungumza na waandishi wa habari katika
banda la baraza hilo kando ya Mkutano wa Mawaziri wa Afya na UKIMWI wa
nchi za SADC unaofanyika kwenye ukimbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
jijini Dar es salaam.
Msajili wa Baraza la Famansia
nchini, Elizabeth Shekalaghe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wafanyakazi wa baraza hilo katika banda la baraza hilo kando ya Mkutano
wa Mawaziri wa Afya na UKIMWI wa nchi za SADC unaofanyika kwenye ukimbi
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
……………………………………………
Msajili wa Baraza la Famansia
nchini, Elizabeth Shekalaghe amesema baraza hilo linashiriki katika
...mkutano wa mawaziri wa afya na UKIMWI wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya
SADC kuona ni mambo gani yatakayojadiliwa katika mkutano huo ili na wao
waone namna nzuri ya kuibua hoja ya wataalamu wa mabaraza ya famasia
katika nchi hizo watakavyoanzisha ushirikiano na kubadilishana utaalamu
hapo baadaye.
Bi. Elizabeth Shekalaghe
ameyasema hayo katika banda la baraza hilo kwenye maonesho yanayoendelea
kando ya mkutano wa mawaziri wa Afya na UKIMWI wa nchi za SADC
unaofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es
salaam.
Amesema kwa upande wa Mabaraza
ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)kumekuwa na ushirikiano
mkubwa kwa wataalam wa Famasia wa nchi hizi ili kuhakikisha dawa
haziuzwi wala kutolewa kiholela kwa watumiaji.
“Kama wataalamu wa Famasia
katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)mabaraza yetu yamekuwa
yakikutana na kufanya vikao mbalimbali ili kujadili changamoto
zinazowakabili wataalamu wa Famasia na kuona ni namna gani tunaweza
kupiga hatua katika utaalamu wa huduma hiii muhimu katika afya”. Amesema
Bi. Elizabeth Shekalaghe
Ameongeza kuwa kama wataweza
kuanzisha ushirikiano huo kwa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za
SADC pia hapo baadae itakuwa ni hatua muhimu sana kufikiwa kwani
itaweza kuongeza wigo wa kubadilishana uzoefu na utaalam wa shughuli za
wafamasia katika mabaraza ya nchi za ukanda huo.
Hapa nchini sheria inataka kila
duka la famasi kuwa na mtaalamu wa famasia mmoja. hivyo wafamasia ni
humuimu sana serikalini pamoja sekta binafsi katika huduma ya afya ,
takwimu zinaonesha mwaka 2013 kulikuwa na wafamasia 350 na kufikia
mwaka jana wamefikia wafamasia 1400 jambo ambalo linaonesha umuhimu wa
kuwepo kwa wataalamu wa famasia na wanatakiwa kuongezeka zaidi ili
kuboresha mazingira ya huduma hii.
No comments :
Post a Comment