Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na Wahitimu na watumishi wa Chuo cha
Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma, katika mahafali ya
33 ya Chuo hicho ambapo aliuagiza uongozi wa chuo hicho kuongeza juhudi
katika masuala ya tafiti zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali za
maendeleo na kupunguza umaskini.
Kamishina Msaidizi wa Bajeti
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Pius Mponzi, akitoa neno la
kumkaribisha mgeni rasmi wa mahafali ya 33 Chuo cha Mipango na Maendeleo
Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), kwa niaba ya Katibu Mkuu waWizara
hiyo.
Mkuu wa Chuo cha Mipango na
Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya akitoa hotuba katika Mahafali ya
33 Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha
Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma, wakimsikiliza kwa
makini Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo
pichani) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 33 ya chuo
hicho.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akimtunuku Shahada ya Mipango na Usimamizi wa
Mazingira mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini
Kampasi Kuu ya Dodoma, katika Mahafali ya 33 ya chuo hicho ambapo
aliwasihi wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kujiajiri.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha
Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma wakivaa kofia baada
ya kutunukiwa Astashahada na Shahada mbalimbali katika Mahafali ya 33 ya
chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere chuoni hapo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akipokea zawadi ya mipira kutoka kwa Mkuu wa
Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya katika
Mahafali ya 33 ya Chuo hicho Kampasi Kuu ya Dodoma, mipira hiyo
imetengenezwa katika kiwanda cha kujenga kiwanda cha kuchakata na
kutengeneza bidhaa za ngozi katika kijiji cha Idifu Wilaya ya Chamwino,
Mkoa wa Dodoma ambapo Chuo kimewekeza jumla ya shilingi milioni 396.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha
Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya wafuatilia kwa karibu
matukio mbalimbali ya kutunukiwa Astashahada na Shahada mbalimbali
katika Mahafali ya 33 ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa
Mwalimu Nyerere chuoni hapo.
Jumuiya ya Chuo
cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma, wakimsikiliza
Mkuu wa Chuo hicho Prof. Hozen Mayaya, akitoa hotuba wakati wa Mahafali
ya 33 ya Chuo hicho ambapo wahitimu 3,182 wa,etunukiwa Astashahada na
shahada mbalimbali.
(Picha na Farida Ramadhani-Wizara ya Fedha na Mipango)
…………………..
Benny Mwaipaja, Dodoma
NAIBU Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amekitaka Chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini, kutafiti kwa kina namna wananchi wanavyoweza
kuondokana na
umasikini wa kipato pamoja namna Miradi mbalimbali ya
Serikali inavyoweza kutekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia thamani ya
fedha kuliko ilivyo sasa.
Dkt. Kijaji
ametoa rai hiyo wakati akiwatunuku astashahada na shahada mbalimbali
wahitimu 3,182 Wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kampasi ya
Dodoma wakati wa sherehe za mahafali ya 33 ya chuo hicho.
Amesema kuwa
matokeo ya tafiti hizo yataisaidia Serikali na Jamii kwa ujumla kupanga
mikakati ya namna ya kukabiliana na umasikini wa wananchi hususan wa
vijijini pamoja na kuharakisha maendeleo ya nchi kwa kuhakikisha kuwa
miradi inayotekelezwa na Serikali inakuwa na tija.
Kwa upande wake
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ni
Kamishna Msaidizi wa Bajeti Bw. Pius Mponzi amemwahidi Dkt. Ashatu
Kijaji, kwaniaba ya Baraza la Chuo hicho kwamba wataongeza jitihada
katika eneo la utafiti na kuhakikisha kuwa matokeo ya utafiti huo
yanawafikia wananchi kwa lugha rahisi
Naye Mkuu wa Chuo
hicho cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya amesema
chuo chake kimetimiza miaka 40 tangu kianzishwe na kimepata mafanikio
makubwa kwa kutoa wahitimu mahili na wenye kukidhi mahitaji ya soko.
Amebainisha kuwa
Chuo kimeongeza idadi ya kozi kutoka kozi moja mwaka 1980 hadi kufikia
kozi 25 mwaka huu, huku idadi ya wanachuo wanaodahiliwa nayo imeongezeka
kutoka wanachuo 13 mwaka huo hadi kufikia wanachuo zaidi ya elfu 11
mwaka huu.
No comments :
Post a Comment