Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka,
akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kuusu masuala ya Fidia kwa
Wafanyakazi yaliyotolewa kwa Waajiri kutoka sehemu mbalimbali nchini na
kufanyika jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Bw,
Deo Ngowi kutoka kitengo cha Sheria Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF), akiwasilisha mada kuhusu Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi.
Bw.Pascal
Rischard kutoka Kitengo cha Usajili na Uwasilishaji Michango WCF,
akiwasilisha mada kuhusu namna ya kujisajili na kuwasilisha michango
kupitia Portal ya WCF
![]() |
| Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, |
![]() |
| Meneja Madai Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akiwasilisha mada kuhusu Mafao yatolewayo na WCF.
|
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia mafunzo hayo.
Maafisa
wa juu wa WCF, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, Bw. Deo Ngowi kutoka Kitengo cha Sheria na
Bw. Pascal Richard kutoka Kitengo cha Usajili na Uwasilishaji Michango WCF
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia mafunzo hayo. NA Khalfan Said
MKURUGENZI
Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka
amewaambia waajiri nchini kuwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi sio hiari bali
ni lazima.
ni lazima.
Dkt.
Mlimuka ameyasema hayo Alhamisi Novemba 28, 2019 jijini Dar es Salaam
wakati akifungua mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na ATE na kuwaleta
pamoja waajiri kutoka sehemu mbalimbali nchini ili kujifunza kuhusu
masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.
“Naomba
tuelewane toka mapema, siyo hiari kujiunga na Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi hilo ni takwa la kisheria Mfuko huu uko pale kisheria na ni
vema likaeleweka mapema.”Alisema Dkt. Mlimuka
Alisema
Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kiko kwa maslahi ya waajiri lakini pia
kwa maslahi ya waajiriwa (wafanyakazi) kwani wameajiriwa ili kufanya
shughuli mbalimbali na wanaweza kuumia au kupatwa na madhara yoyote
wakati wakitekeleza
majukumu yao na ndio maana upo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ambao umeundwa maalum kushughulikia masuala hayo.
majukumu yao na ndio maana upo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ambao umeundwa maalum kushughulikia masuala hayo.
“Niwashukuru sana viongozi wa WCF kwa kuja hapa leo
kutupatia mafunzo, sisi waajiri tutanufaika vya kutosha na mafunzo haya ambayo yataweza kujibu maswali yaliyo mengi kutokana na changamoto mbalimbali.” Alibainisha Dkt. Mlimuka.
kutupatia mafunzo, sisi waajiri tutanufaika vya kutosha na mafunzo haya ambayo yataweza kujibu maswali yaliyo mengi kutokana na changamoto mbalimbali.” Alibainisha Dkt. Mlimuka.
Alisema,hapo
zamani malipo ya Fidia kwa Mfanyakazi aliyeumia yalikuwa kidogo sana,
na ndio maana Serikali ikaanzisha Mfuko huu ambao umesaidia sana katika
kutatua changamoto zilizokuwa zikitukabili kutokana na masuala ya Fidia.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini,
Dkt. Abdulsalaam Omary alisema, Waajiri wanao wajibu wa kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wao unapewa umuhimu wa kwanza na ndio maana WCF inatoa elimu mara kwa mara.
“Ifahamike
kuwa sisi WCF wajibu wetu wa msingi ni kulipa fidia stahiki na kwa
wakati kwa mfanyakzi aliyeumia, kuugua au kufariki wakati akitekeleza
wajibu wake wa kazi… kusajili na kupokea michango kutoka kwa waajiri
walio katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara, lakini pia tunalo
jukumu la kisheria la kukuza mbinu za kuzuia ajali na vifo kazini kwa
kutoa elimu kwa waajiri lakini pia wafanyakazi wenyewe na hiki ndicho
tunachokifanya hapa leo.” Alisema Dkt. Omary wakati akiwasilisha mada yake ya namna ya kudai Fidia.
Washiriki
hao walipatiwa mafunzo mbalimbali yakiwemo Sheria iliyoanzisha Mfuko,
Kujisajili na jinsi ya kuwasilisha michango WCF na namna ya kuwasilisha
madai ya Fidia, lakini pia Mafao yanayotolewa na Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi.












No comments :
Post a Comment