Saturday, November 30, 2019

BODI YA URATIBU WA NGOs YATEMBELEA MIRADI YA PLAN INTERNATIONAL JIJINI MWANZA



Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao akifafanua jambo kwa vijana wa kikundi cha Shilabela wanaonufaika na mradi wa Vijana Maisha ni Kazi unaotekelezwa na Shirika la Plan International Buhongwa jijini Mwanza wakati Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali  ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.

Mwezeshaji kutoka Shirika la Amani Girls Home Bw. Mang’olo Shoma Bahati akieleze jinsi Mradi wa Vijana Maisha ni Kazi unaotekelezwa na Shirika la Plan International ulivyowasaidia vijana wa Kikundi cha Shilabela cha Buhongwa wakati Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali  ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika.

Afisa Miradi kutoka Shirika la Plan International Bw. Nicodemas Gachu akielezea kuhusu utekelezaji wa Miradi inayotekelezwa na Shirika hilo wakati Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ilipotembelea Miradi inayotekelezwa na Shirika hilo mkoani Mwanza katika ufuatiliaji wa mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Richard Faustine Sambaiga (Mwenye koti) akikabidhi mchango wa jamii kwa mmoja wa mjumbe wa kikundi cha Shilabela kilichopo Buhongwa jijini Mwanza wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.

No comments :

Post a Comment