Waziri wa Madini, Doto Biteko
akiwakaribisha wajumbe kutoka Kampuni ya Mantra Tanzania na wataalamu wa
Wizara katika kikao kilichojadili juu ya uchimbaji wa madini ya uranium
nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na
Mipango, Augustine Ollal akihoji jambo wakati wa kikao baina ya wizara
na Kampuni ya Mantra Tanzania kilichofanyika katika Ofisi ya Waziri wa
Madini Doto Biteko (katikati) mapema leo tarehe 1 Oktoba, 2019
Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra
nchini Frederick Kibodya akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya
kampuni hiyo na wizara kilichoongozwa na Waziri wa Madini Doto Biteko.
Waziri wa Madini, Doto Biteko
akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uranium One
Alexander Ryabchenko akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya wizara
na kampuni hiyo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko na
wajumbe walioshiriki kikao baina ya wizara na kampuni ya Mantra Tanzania
wakifurahia jambo wakati kikao hicho kikiendelea.
Waziri wa Madini, Doto Biteko
akizungumza kwa simu na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Nchini(Jina halikupatikana) kuomba nafasi kwa ajili ya uongozi wa
kampuni ya Mantra Tanzania kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala
yanayosimamiwa na mamlaka hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Mantra Tanzania Alexander Ryabchenko akizungumza jambo wakati wa kikao
baina ya Wizara na kampuni hiyo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko
akiagana kwa kushikana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Uranium One Alexander Ryabchenko mara baada ya kumaliza kikao baina ya
wizara na kampuni hiyo. Katikati ni Rais wa kampuni hiyo Vasiliy
Konstantinov
…………………….
Waziri wa Madini Doto Biteko,
ameitaka kampuni ya Mantra Tanzania kuipa nafasi ofisi yake ili kuweza
kujiridhisha endapo maombi ya kusitisha kuanza kwa shughuli za uchimbaji
wa
madini hayo una tija kwa kampuni na Taifa.
Waziri Biteko ametoa kauli hiyo
leo wakati wa kikao baina ya Wizara na uongozi wa Kampuni hiyo ulioitaka
wizara kuridhia ombi la kusogeza mbele shughuli za uzalishaji wa madini
hayo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2020 mpaka 2024.
Akizungumza hoja hiyo
iliyowasilishwa katika kikao hicho, Waziri Biteko alihoji uhakika bei ya
madini hayo ifikapo mwaka 2024 katika soko la dunia la endapo utakuwa
wakuridhisha na kuwataka kuwasilisha data zao ili ofisi yake iweze
kuzifanyia kazi.
“Ni kiashira gani kinachowaonesha kuwa ifikapo 2024 kutakuwa na ongezeko la thamani kwa madini ya urani?” Biteko alihoji.
Aidha, Biteko aliutaka uongozi wa
Kampuni hiyo kuwasilisha mchanganuo unaoonesha ongezeko la thamani ya
madini ya urani ifikapo 2024 ili wataalamu wa wizara wafanyie kazi na
kuishauri wizara juu ya kuridhia au kutoridhia maombi hayo.
Akizungumzia juu ya maamuzi
yaliyofikiwa na kampuni hiyo, Rais wa Kampuni ya Mantra Tanzania,
Vasiliy Konstantinov alisema bei ya kuuza madini hayo kwenye soko la
dunia imeshuka jambo ambalo litapelekea kampuni na serikali
kutokunufaika na uwekezaji huo kutokana na kuwekeza kwa hasara.
Konstantinov alisema kuwa kampuni
imeamua kufika na kukaa na wizara ili kupata msaada na kuhakikishiwa
uhakika wa kuendelea na uwekezaji huo mara baada ya thamani ya madini
hayo kuongezeka ili kuwawezesha kuwekeza kwa faida.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
leseni na Tehama kutoka Tume ya Madini, Yahya Samamba alihoji uamuzi wa
Kampuni hiyo kuendelea na uwekezaji ifikapo 2024 endapo hakutokuwa na
mabadiliko ya kuridhisha katika soko la dunia.
Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Mantra Tanzania, Alexander Ryabchenko alisema kwa sasa
kampuni hiyo iko katika utafiti wa kutafuta njia rahisi isiyotumia
gharama kubwa za uwekezaji ili kuifanya kampuni hiyo kuendelea na
uzalishaji mara baada ya muda huo kufika hata kama bei ya madini hiyo
haitabadilika.
Mantra Tanzania ni kampuni ya uchimbaji mkubwa wa Madini nchini iliyotolewa na Wizara ya Madini mwaka 2013.
No comments :
Post a Comment