
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Selemani Jafo
amesema kuwa Kuna halmashauri 121 hazikufikia lengo walilowekewa la
kuhakikisha
wanakusanya zaidi ya asilimia 25 ya makisio yake.
Huku bajeti
iliyoidhinishwa ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa mwaka huo ni sh.
Bilioni 765.48, huku robo ya kwanza July hadi Septemba,2019, Halmashauri
zimekusanya sh. Bilioni 166.24 sawa na asilimia 22 ya makisio ya mwaka.
Waziri Jafo
ameyabainisha leo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya mapato ya
vyanzo vya ndani vya halmashauri kwa kipindi Cha Julai Hadi Septemba kwa
mwaka wa fedha 2019/2020.
Amesema halmashauri zote
zilitakiwa kukusanya mapato kwa asilimia 25 ya makisio yake ya mwaka,
hata hivyo kuna halmashauri zipatazo 121 hazikuweza kufikisha asilimia
25, wakati zilizofikia lengo zikiwa 54 tu.
“Nitoe salamu kwa
Wakurugenzi na huu ni ujumbe mwingine msione kwa wenzenu waliopita,
niwaambie ukusanyaji wa mapato ndio kigezo kinachowafanya mkae kwenye
nafasi zenu, mmeteuliwa kusimamia mapato” amesema Jafo.
Amewataka kutumia mwezi
Oktoba hadi Disemba kujitathmini na kuhakikisha Wakurugenzi hao
wanafikia malengo waliyowekewa na kufikisha asilimia 25 za makisio yao.
Pia amewaonya
Wakurugenzi wote wazembe ambao wanasuasua kwenye ukusanyaji wa mapato na
kutaka wajitathmini kwa miezi mitatu ijayo
Ameongeza kuwa ”
Mkurugenzi wa Buhigwe anapaswa kujitathmini na naomba Katibu Mkuu
uliweke vizuri kwa sababu nilienda Buhigwe hata utekelezaji wa miradi ya
maendeleo unasuasua, hata miradi iliyopelekewa fedha na Serikali kuu”
amesema.
Kuhusu hali ya
ukusanyaji, Waziri Jafo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imekuwa
ya kwanza kiasilimia kwa kuwa imekusanya imekusanya mapato kwa asilimia
52 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka huu, huku halmashauri ya
Wilaya ya Kyerwa ikishika nafasi ya mwisho kwa kukusanya asilimia 3 ya
makisio yake.
Wakati Halmashauri ya
Jiji la Dodoma imeongoza kwa makusanyo ya mapato mengi zaidi kuliko
halmashauri zote kwa kukusanya Bilioni 13.10, huku halmashauri ya Wilaya
ya Buhigwe ikishika nafasi ya mwisho kwa kukusanya sh.milioni 35.15.
Aidha Waziri Jafo
amebainisha kuwa Mkoa wa Dar es saalam umeongoza kwa wingi wa mapato
ambapo umekusanya Bilioni 39.53, huku Mkoa wa Kigoma ikishika nafasi ya
mwisho kwa kukusanya Bilioni 2.12 katika kipindi hicho.
No comments :
Post a Comment