
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania
Foundation Rosalynn Mworia akimuelekeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe jinsi mfumo wa Instant Schools
unavyofanya kazi, Vodacom Tanzania Foundation imekabidhi kompyuta
mpakato, router na kuunganisha intaneti yenye tahamani ya Shilingi 67m
kwa shule 24 wilayani Urambo.
……………………….
· Yaonyesha njia katika maendeleo ya teknolojia ya Kidijitali kupitia mfumo wa e-learning
· Zaidi ya wanafunzi 7,000 kunufaika na msaada huo.
Oktoba 19, 2019 Urambo.
Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano nchini,
Vodacom
Tanzania Plc, kupitia taasisi yake ya Vodacom Tanzania Foundation leo
imetoa msaada wa kompyuta na Kipanga njia (Router) vilivyounganishwa
katika intaneti kwa shule 14 za Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora. Msaada
huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi 67,634,000 ni sehemu ya mpango endelevu wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa taarifa muhimu katika sekta ya elimu.
Hii ni sehemu ya ushirikiano wa
Vodacom na mfuko wa pamoja wa huduma za Mawasiliano (UCSAF) wa kutoa
elimu shuleni kwa kutumia miundombinu bora ya teknolojia ya mawasiliano
ya Vodacom kote nchini . Kupitia ushirikiano huo, jumla ya shule 300 na
hasa zilizoko vijijini zitapata kompyuta zilizounganishwa katika
intaneti bure.
Akipokea msaada huo, katika shule ya Sekondari Urambo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack
Aloyce Kamwelwe, alisema msaada huo wa kompyuta ni hatua muhimu
kuelekea mchakato wa maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano ya
kidijitali.
“Maendeleo
ya kuelekea kwenye matumizi ya dijitali yanaonesha kuwapo mafanikio
kutokana na uwepo wa kompyuta kama hizi katika shule zetu sambamba na
kasi ya matumizi ya simu za mkononi nchini,” alisema Waziri Kamwelwe.
“Shule ni mahala pazuri pa kuanzia kufundisha matumizi ya kompyuta katika maisha ya kila siku. Kompyuta
zikiwa shuleni hazitatumika kwa wanafunzi pekee kujifunza matumizi
yake, lakini pia walimu kutumia kompyuta hizi kupata ujuzi zaidi na
kuboresha uwezo wao wa kufundisha. Walimu pia watatumia muda huo
kuboresha ujuzi wao ili kwenda sambamba na ulimwengu wa kidijitali na
kupata maarifa Zaidi,” aliongeza Mh Kamwelwe.
“Tunaamini kwamba kompyuta hizi ni
hatua nyingine katika mchakato wa mabadiliko ya kidijitali.
Tunawashukuru Vodacom Tanzania Foundation kwa msaada wao mzuri,” alisema
Kamwelwe.
Mkurugenzi wa Vodacom Foundation, bi Rosalynn Mworia, alisema msaada
huo ni sehemu ya ajenda ya Vodacom Foundation yenye lengo la kusaidia
sekta ya elimu ili kutoa elimu bora na kuhakikisha wanafikia malengo ya
millenia na ajenda ya kitaifa kama sehemu ya mradi wa shughuli za
kijamii.
“Fursa za
kidijitali ni nishati muhimu katika uchumi unaokua, zina matokeo ya
haraka katika uchumi na jamii kwa ujumla. Kwa pamoja zinachangia ukuaji
wa uchumi, kuongeza mianya ya ajira pia ina mchango mkubwa katika
kupunguza umasikini, huku ikitoa mwanya katika kuchochea ukuaji wa sekta
muhimu kama vile elimu na afya,” alisema bi Mworia.
“Vodacom
imeamua kuweka nguvu katika maendeleo kidigitali Tanzania. Ndiyo maana
tunajivunia kutoa msaada huu leo ambao unajumuisha kompyuta, rota vyote
vikiunganishwa katika mtandao vikiwa na thamani za zaidi ya shilingi
milioni 67 katika shule 14 wilayani Urambo ambayo inategemea kuwafikia
zaidi ya wanafunzi 7,000,” alisema Mworia.
“Vodacom
imejikita zaidi katika kukuza maendeleo ya kidijitali, mawasiliano na
ubunifu nchini. Tunataka kuwasaidia wanafunzi ili waende sambamba na
zama hizi za kidijitali tulizomo kwa sasa na kuwashawishi zaidi kutokuwa
watumiaji tu, bali kushiriki kikamilifu katika fursa za kidijitali.
Tukio la leo ni mwendelezo wa utoaji wa Kompyuta chini ya ushirikiano wa
Vodacom Tanzania Foundation na UCSAF kwa shule za Tanzania Bara na
Visiwani,” alisema Mworia
Wiki iliyopita,
Vodacom ilitoa kompyuta na router zilizounganishwa na intaneti yenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 48 kwa shule 10 Mkoani Simiyu.
Kompyuta hizi
zitawezesha shule hizo kupata taarifa mbalimbali za elimu kutoka katika
mfumo wa kidijitali kupitia katika muundo wa foundation yetu na hivyo
kuhamasisha usomaji wa kidijitali.
Vodacom imekuwa
mstari wa mbele kuunga mkono maendeleo ya teknolojia shuleni kupitia
mpango wa Instant Schools, ambapo imetoa kompyuta mpakato na za kawaida
75 katika wa shule za sekondari za Kambangwa, Makumbusho, Mtakuja na
Kinyerezi.
No comments :
Post a Comment