
**********************
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) katika jitihada za kuboresha huduma ya Afya linatarajia
kuzindua Idara mpya ya huduma ya Tiba ya Dialysis katika Hospitali Kuu
ya Jeshi, Lugalo.
Shughuli za uzinduzi huo
zinatarajia kufanyika kesho Jumatano tarehe 23 Oktoba, 2019 kwenye
Hospitali kuu ya Jeshi Lugalo iliyopo Jijini Dar es Salaam kuanzia saa
mbili na nusu (2:30) asubuhi. Mgeni rasmi katika shughuli hiyo
anatarajiwa kuwa Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Ukiwa mdau katika Tasnia ya
Habari, JWTZ linakialika chombo chako cha Habari kwenye hafla hiyo
muhimu ili kuuhabarisha umma juu ya huduma hiyo kupatikana Jeshini.
No comments :
Post a Comment