
MKUU wa Kanda ya Mashariki wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akimkabidhi
kitabu cha mongozo wa mawasiliano kwa mwananchi aliyetembelea maonesho
ya wiki ya viwanda mkoa wa pwani yanayofanyika katika viwanja vya ofisi
ya mkuu wa mkoa.

Afisa Mwandamizi wa Mitambo wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki Kenneth Chitemo
akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TCRA katika maonesho
ya wiki ya viwanda mkoa wa Pwani yanayofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Pwani.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akiwa picha pamoja na wadhamini wa maonesho ya viwanda.

Wakuu wa Taasisi wakiwa katika Kongamano la wiki ya viwanda mkoa wa Pwani yanayofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
*****************
Na Mwandishi WETU
Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imeshiriki maonesho ya
wiki ya viwanda mkoa wa Pwani katika utoaji wa elimu ya mawasiliano
pamoja na
usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
Akizungumza
katika maonesho hayo Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi
Lawi Odiero amesema kuwa katika maonesho hayo wananchi watembelee banda
la TCRA kuweza kupata elimu namna ya kutumia l simu katika kupata
maendeleo ya Taifa.
Mhandisi Odiero
amesema kuwa uchumi wa viwanda unakwenda na mawasiliano ya simu na
kutaka wadau kutumia simu katika biashara zao kwa kutangaza biasha kwa
kutumia simu hizo.
Aidha amesema
TCRA iko katika kampeni ya kuhamasisha wananchi kujisajili kwa laini za
simu kwa lama za vidole kwa muda uliopangwa na usajili huo utafungwa
Desemba 31 mwaka huu.
“Tunataka
wananchi wajisajili simu zao kwa alama za vidole kwa muda uliopangwa na
wasije wakapata usumbufu wakati zoezi hilo likiwa limefungwa kwa laini
za simu kutopata mawasiliano.amsesema Mhandisi Odiero.
Mhandisi Odiero
amesema kuwa Kanda ya Mashariki ya TCRA itapita Wilaya zote zilizo
katika kanda hiyo katika kutoa elimu ya usajili wa laini za simu kwa
alama za vidole pamoja na huduma nyinginezo za bidhaa za mawasiliano.
Hata hivyo
amesema kuwa wananchi waepuke kufanya maawsiliano na watu wasiowajua kwa
kuwaomaba fedha ni mpaka pale watakapojiridhisha na katika mawasiliano
kwani baadhi yao wanafanya utapeli.
No comments :
Post a Comment