Waziri Mkuu,Mh.Kassim Majaliwa
alikabidhi Tuzo kwa Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TBL,Amanda Walter
kwa niaba ya Kampuni katika hafla hiyo
Baadhi ya Wafanyakazi wa TBL wakifurahia mafanikio ya Kampuni wakati wa hafla hiyo.
Baadhi
ya wawakilishi kutoka makampuni yaliyoshinda na viongozi wa Serikali na
CTI, wakiwa katika Picha ya pamoja na Waziri Mkuu, Mh.Kassim
Majaliwa,wakati wa hafla hiyo.
Baadhi
ya wawakilishi kutoka makampuni yaliyoshinda na viongozi wa Serikali na
CTI, wakiwa katika Picha ya pamoja na Waziri Mkuu, Mh.Kassim
Majaliwa,wakati wa hafla hiyo.
********************************
Kampuni ya TBL imeendelea kung’ara
baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika sekta ya
viwanda vya vinywaji
kwenye tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora iliyofanyika katika hoteli ya
Serena, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo
ambayo hutayarishwa na Shirikisho la wenye Viwanda nchini (CTI), alikuwa
ni Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Mbali na kuibuka mshindi wa
kwanza katika sekta ya viwanda vya vinywaji, TBL pia iliibuka mshindi wa
pili katika sekta ya viwanda.
Akiongea kuhusu ushindi huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Philip Redman alisema “TBL tumejipanga
kuendesha viwanda nchini Tanzania kwendana na viwango vya kimataifa,
ushindi huu unadhihirisha dhamira yetu hiyo na ndio maana pia viwanda
vyetu vinashikiria rekodi ya kuwa miongoni mwa viwanda bora duniani”.
Redman, alisema kuwa TBL ni mdau
mkubwa wa kuunga jitihada za Serikali za kuifanya Tanzania nchi ya
viwanda sambamba na kufanya uwekezaji unaochagia kukuza shughuli za
kijamii na uchumi wa nchi “Mpango wetu wa kununua malighafi kwa asilimia
70% nchini kama vile Shahiri,mtama na mahindi utafanikisha kuinua
maisha maisha ya wananchi kwa haraka sambamba na kufikia uchumi wa kati
hadi ifikapo mwaka 2025”, alisema.
TBL pia ni kampuni ambayo imekuwa
ikiendesha biashara zake kwa kuzingatia taratibu za nchi na inafanya
kazi na wadau mbalimbali sambamba na kutoa kipaumbele cha kutumia
malighafi za ndani kwa ajili ya kutengenezea chapa mbalimbali za bia
ambazo zinakubalika kwa kiasi kikubwa kwa wateja katika masoko ya
ndani.
Ikiwa uwezekaji wake umewezesha
kuchagia zaidi ya shilingi bilioni 500 za mapato ya Serikali kupitia
kukusanya na kulipa kodi na kufanikisha miradi ya kusaidia jamii,TBL pia
imekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika teknolojia za
kisasa,wafanyakazi wake na wadau wake inaoshirikiana nao katika
biashara.
No comments :
Post a Comment