
Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa na Makamu wa Rais wa ‘Asian
Infrastructure Investment Bank’ Katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye
ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) akiwa katika mazungumzo na Bw. Danny
Alexander Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment
Bank’ yaliyofayika katika ukumbi wa mikutano wa Ubalozi wa Tanzania
Jijini Washington DC. Kushoto kwa Mhe.Waziri ni Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana, Dkt.Yamungu Kayandabila.

Makamu wa Rais wa ‘Asian
Infrastructure Investment Bank’ akiwa katika picha ya pamoja na Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) kulia, na Waziri
wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Mohammed Abdiwawa. Kulia kwa Mhe.
Mpango ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Mashimba Ndaki
na kushoto kwa Mhe.Abdiwawa ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof.
Florens Luoga.
***************************************
Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington DC
Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) amefanya mazungumzo na
Makamu wa Rais
wa ‘Asian Infrustructure Investment Bank’ Bw. Danny Alexander jijini
Washington DC. Katika mazungumzo na Benki hiyo wamekubaliana kusaidia
katika miardi endelevu ya Miundombinu kama Barabara na Reli.
Mazungumzo hayo ambayo pia
yalihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar,Mhe.Mohammed Abdiwawa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof.
Florens Luoga na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt.Yamungu Kayandabila
yalikuwa na lengo la kuangalia fursa ambazo Tanzania inaweza kunufaika
kutoka katika Benki hiyo.
No comments :
Post a Comment