Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi
akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi ya ushauri
wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) Bwana Stephen Karangizi mazungumzo hayo yamefanyika katika
makao makuu ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Abidjan Nchini Ivory
Coast.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb)
akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi ya ushauri wa
kishheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) mara baada ya kumaliza majadiliano kuhusu kuandaa
mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada
wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP)
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) akiwa
katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi
ya ushauri wa kishheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) mara baada ya kumaliza majadiliano kuhusu kuandaa
mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada
wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP). Wa
pili kutoka kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt.
Yamungu Kayandabila.
Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi
wa Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bwana Stephen Karangizi(kulia)
akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) wakati wa majadiliano
kuhusu kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum
na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu
wa serikali (DPP) anayefuatia baada ya Bw. Stephen Karangizi ni Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila.
*****************
Na Mwandishi wetu, Abidjan,Ivory Coast.
Tanzania na
Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki
ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimekubaliana kuandaa mkakati maalum kwa
ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa
Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) hususani katika
kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania
na ya Kimataifa katika maeneo ya madini, biashara na usuluhishi na
makampuni ya Kimataifa pamoja na mafuta na gesi.
Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi
ameyasema hayo mara baada ya majadiliano na Afisa Mtendaji Mkuu na
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) Bwana
Stephen Karangizi mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki
ya Maendeleo Afrika (AfDB) Abidjan Nchini Ivory Coast.
Prof. Kabudi
amesema kuwa lengo la majadiliano hayo ni kuisaidia Tanzania kuweka
mikakati kuimarisha sekta ya Sheria ikiwa ni pamoja na kuiongezea uwezo
ofisi ya mwanasheria mkuu wa Tanzania hasa baada ya mabadiliko makubwa
yaliyofanywa ya muundo mpya wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ili
kuiwezesha kutoa ushauri wa kina na wa kitaalam kwa serikali lakini pia
kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya
Tanzania na ya Kimataifa.
Ameongeza kuwa
maombi ya Tanzania kwa taasisi hiyo kwa ajili ya kuisaidia ofisi ya
mwanasheria na wakili mkuu wa serikali yamekamilika na kinachosubiriwa
hivi sasa ni kuwasilisha maombi hayo kwa kikao cha bodi ili utekelezaji
uanze.
Ameongeza kuwa
eneo jingine ambalo Tanzania inahitaji msaada kutoka kwa Tanzania na
Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki
ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ni kuhusu kuisaidia Tanzania katika hatua
iliyoichukua ya kutunga sheria mpya ya usuluhishi wa migogoro ya
kimataifa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo kipya cha
kusimamia usuluhishi wa migogoro.
Katika eneo hilo
Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki
ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itatoa wataalamu kusaidia Tanzania
kupitia miswaada ambayo imeandaliwa na serikali pia kuandaa andiko la
namna kituo hicho kitawekwa Tanzania na kukidhi matakwa ya kimataifa.
Kwa uoande wake
Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria
ya Afrika Bw Stephen Karangizi amesema wamepokea ombi hilo na kwamba
wanasubiri maamuzi ya kikao cha bodi ili kuweza kuanda program maalum
kwa ajili ya kuimarisha na kuendeleza ofisi ya mwanasheria mkuu wa
serikali.
Ameongeza kuwa
nchi nyingi za Kiafrika zimeshindwa katika usuluhishi wa migogoro
hususani ya kibiashara,madini,mafuta na gesi na maeneo mengine na
kuongeza kuwa suala hilo linapaswa kuwekewa mkakati maalum na
kutekelezwa kwa haraka ili kuepuka makosa yaliyokwisha kufanywa katika
siku zilizopita.
Taasisi hiyo ya
ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyo chini ya Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) ilianzishwa kutokana na ombi la Mawaziri wa fedha
kutoka Afrika kwa lengo la kuzisaidia Nchi za Afrika kujijengea uwezo
katika masuala ya kisheria hususani katika madini,mafuta na gesi pamoja
na madeni ili kuziwezesha nchi za Kiafrika kuwa na uwanda sawa wa
majadiliano katika ngazi za Kimataifa kuhusu masuala ya kisheria
yanahusu biashara na makampuni ya Kimataifa.
No comments :
Post a Comment