Tuesday, October 1, 2019

TAASISI YA ELIMU HAPA NCHINI YAZINDUA MPANGO WA UGAWAJI NA USAMBAZAJI WA VITABU VYA KIADA KWA SHULE ZA AWALI NA MSINGI



Mkurugenzi mkuu wa Tasisi ya Elimu nchini Dr.Aneth Komba akigawa vitabu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Oster bay jijini Dar es Salaam baada ya uzinduzi wa mpango wa ugawaji na usambazaji wa  vitabu vya kiada kwa shule zinazotumia lugha ya kiingereza kufundishia na kujifunzia Wanafunzi wa shule ya msingi Oster bay jijini Dar es Salaam wakipitia kuvisoma vitabu baada ya uzinduzi wa mpango wa ugawaji na usambazaji wa vitabu vya kiada kwa shule zinazotumia lugha ya kiingereza kufundishia na kujifunzia Mkurugenzi mkuu wa Tasisi ya Elimu nchini Dkt.Aneth Komba akionesha moja ya kitabu   baada ya uzinduzi wa mpango wa ugawaji na usambazaji wa vitabu vya kiada kwa shule zinazotumia lugha ya kiingereza kufundishia na kujifunzia.
***************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wamiliki wa shule binafsi,walimu pamoja wazazi wametakiwa kutumia vitabu vyenye hidhini ya Serikali na kuachana na tabia ya kutumia vitabu ambavyo havitambuliwi na Serikali.
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt.Aneth Komba akizindua kazi ya kusambaza vitabu vya vitabu vya kiada kwa shule zinazotumia lugha ya
kiingereza kufundishia na kujifunzia.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Dkt.Aneth amesema kuwa shule zote zitapewa vitabu bure na vitagawanywa kwa uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi watatu lakini lengo la Serikali ni kufikia kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja.
“Tumeandaa vitabu hivihivi kwa shule za binafsi kwa bei pungufu wakati vitabu ambavyo vitagawiwa kwa shule za Serikali kwa nyuma vimeandikwa (Not for Sale)”.Amesema Dkt.Aneth.
Aidha Dkt.Aneth amesema kuwa Taasisi hiyo inakazi ya kudhibiti ubora wa vitabu hivyo wanakitengo cha udhibiti ubora ambao kazi yake ni kupitia vitabu na nyaraka zote ambazo zimeandaliwa kwenda kwenye shule za Tanzania kianzia ngazi ya awali mpaka vyuo vya Ualimu.
Pamoja na hayo, Dkt.Aneth ametoa wito kwa shule zote ambazo zitapata vitabu hivyo kuvitumia na kuvitunza.
Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Dar es Salaam Bw. George Lukoa amewasihi wadau wa Elimu hasa Wanafunzi wasome kwa bidii ili kuweza kuendana na mfumo wa Elimu bure unaotolewa na Serikali kwani Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kuwezesha Elimu bure kwa wanafunzi hapa nchini.

No comments :

Post a Comment