Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji
Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa
Tanzania, Kassim Majaliwa wakati akifungua Kongamano la Tatu la Mafuta
na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius
Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Kongamano hilo linawakutanisha wadau zaidi ya 592 kutoka Mataifa mbali
mbali ikiwemo Austaralia, Brazili, Canada, China, Visiwa Vya Comoro,
Ghana. Mengine ni Itali, India, Japani, Kenya, Msumbiji, Netherand,
Nigeria, Afrika Kusini, Oman, Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Waziri
wa Nishati na Madini Meldard Kalemani akizungumza wakati wa ufunguzi wa
Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo
cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia
Oktoba 2-3, 2019.
Serikali ya Tanzania ametaja maeneo manne yanayoashiria matumaini ya
ugunduzi wa rasilimali ya Mafuta nchini kwa siku za usoni kupitia
shughuli za utafiti zinazoendelea.
Maeneo aliyoyataja ni pamoja na ya ukanda wa Ziwa Rukwa, Ziwa Tanganyika
na Kitalu cha Eyasi Wembere chenye ukubwa wa kilometa za mraba 19. 2.
Kitalu hicho kinapita katika mikoa ya Arusha, Manyara, Simiyu, Shinyanga
na Tabora.
Dk Kalemali ametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 2, 2019 Jijini Dar es
Salaam, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Mafuta na Gesi.
“Kuanzia eneo la Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa, maeneo ya Pwani ya Tanga
pamoja na Kitalu cha Eyasi Wembere, tunashukuru timu ya wataalamu ya
Uganda inayosaidiana na Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC) katika kusaidia ushauri,” amesema Waziri Kalemani.
Akifungua Mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema
kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wanaokuja katika
sekya ya Mafuta na Gesi.
"Tunawakaribisha wawekezaji zaidi wajitokeze katika sekta hii ili kuweza
kukuza uchumi wa nchi na kuzidi kutoa ajira wa jamii," amesema.
Meza kuu: Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Makamu mwenyekiti wa Chama Watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdulsamad Abdurahim, Waziri
wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib na
Bi. Irene Batete aliyemwakilisha waziri wa Nishati Nchini Uganda.
Waziri wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib
akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi
Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere
(JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Bi. Irene Batete aliyemwakilisha Waziri wa Nishati Nchini Uganda
akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi
Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere
(JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Makamu
mwenyekiti wa Chama Watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania,
Mheshimiwa Abdulsamad Abdurahim ambao ndiyo waandaaji akizungumza wakati
wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania
linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC)
Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Wageni
waalikwa toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la
Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.

na viongozi wawakilishi Mabalozi toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria
Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo
cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia
Oktoba 2-3, 2019.
Wageni
na viongozi wawakilishi Mabalozi toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria
Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo
cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia
Oktoba 2-3, 2019.
No comments :
Post a Comment