***************************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
WENYE Viwanda 173
mkoani Pwani wamethibitisha kushiriki katika maonyesho ya pili ya
viwanda yanayotarajiwa kufanyika octoba 17-23 mwaka huu ,idadi ambayo
bado ni ndogo kukidhi lengo la washiriki 400 lililokuwa limewekwa
kimkoa.
Aidha waliothibitisha
kushiriki katika kongamano la wawekezaji ni 170 ,hivyo mkoa unaendelea
kuwaomba wawekezaji kujitokeza na kuchangamkia fursa hiyo .
Akizungumza na
waandishi wa habari, kuhusiana na tathmini ya maandalizi ya maonyesho na
kongamano hilo ,mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema
, kamati imependekeza kusogeza mbele maonyesho hayo ambapo yatakuwa
octoba 17 hadi 23 badala ya tarehe 1-7 octoba .
Alieleza, kati ya
washiriki waliojitokeza 53 ni viwanda ,wajasiriamali 100 na wenye
viwanda vidogo (SIDO ) 20 ikiwa ni chini ya asilimia 50.
Pamoja na hilo
,Ndikilo alifafanua wanatarajia kuongeza idadi ya wawekezaji
watakaoshiriki kutoka 166 mwaka 2018 hadi kufikia 500.
“Pia inatupasa
tupishe maandalizi kuelekea siku ya kuzima mwenge ,na baada ya hapo
ndipo kutafanyika maonyesho na kongamano hili”
“Waratibu wa
maonyesho hayo watakuwa ni wabobezi wa masuala ya maonyesho kama hayo
kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) pamoja na mamlaka ya maendeleo ya
viwanda (TANTRADE)”
Alieleza, malengo ya
matukio hayo ni kuonyesha kwamba mkoa wa Pwani ,umedhamiria kuwa ukanda
wa viwanda,wenye viwanda kupata masoko ya uhakika,kupanua wigo wa soko
la ndani ya mkoa kufikia kimataifa na ,kuvutia wawekezaji wapya.
Aidha Ndikilo
alifafanua lengo la kongamano hilo ,kuwa ni kuonyesha fursa za uwekezaji
zilizopo mkoani humo kupitia sekta mbalimbali ikiwemo
utalii,uchumi,kijamii,kilimo,uvuvi na viwanda.
“Kufanyika kwa
kongamano hili italeta picha halisi ya fursa zote zilizopo mkoani
Pwani,na kuonyesha namna mkoa ulivyopiga hatua katika sekta ya
viwanda,uwekezaji na fursa za miradi mikubwa ikiwemo mradi mkubwa wa
ujenzi wa uzalishaji umeme megawatts 2,100 STIGO ,huko
Rufiji”alibainisha Ndikilo.
Nae Januarius Maganga wa TSN alisema ,wanakwenda kuratibu maonyesho hayo ikiwa ni maonyesho ya kumi .
Kwa upande wake
,mwakilishi wa mkurugenzi kutoka TANTRADE ,Victor Rugemalila
aliwahakikishia wananchi na mkoa kwamba ,wamejipanga kuona namna bidhaa
inakua na kuleta maendeleo ya wenye viwanda na kuratibu kwa ufanisi
mkubwa maonyesho hayo.
No comments :
Post a Comment