Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt.
Damas Ndumbaro akisoma taarifa kwenye kikao kati ya Wizara na Kamati ya
Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kulia ni Katibu Mkuu
wa Wizara Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe
Naibu Waziri Mhe. Dkt.
Ndumbaro leo ameongoza ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki kwenye kikao kati ya Wizara na Kamati ya Bunge ya
Kudumu ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika ukumbi
mdogo wa mikutano wa Bunge jijini Dodoma. Kamati
ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ikiongozwa na
Mwenyekiti wake Mhe. Musa Azzan Zungu (MB), kwa pamoja wameipongeza
Wizara kwa kutekeleza vyema mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo
katika vikao vilivyopita, sambamba na utekelezaji mzuri wa vipaumbele na
malengo ya Wizara.
Kikao hicho kilitoa fursa kwa Wizara
kuwasilisha kwa kamati taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu
yake. Aidha, kikao hicho hutoa fursa kwa kamati kupokea na kujadili
taarifa za Wizara pamoja na kutoa mapendekezo yake kuhusu masuala
mbalimbali. |
No comments :
Post a Comment