
**********************************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkutano wa Sadc ambao unaendelea
umebeba madhumuni ya kuangalia mwenendo mzima wa hali ya mazingira na
mabadiliko ya Tabianchi ikiwa ni pamoja na kubainisha utekelezaji wa
mikakati ya hifadhi ya usimamizi wa mazingira
Mkutano huo kesho utaingia hatua
ya pili ya makatibu wakuu baada ya wataalamu kumaliza ngwe yao jana na
utafunguliwa na Waziri mwenye dhamana ya utalii Dkt.Khamis Kigwangalah
kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa Aicc jijini hapa
Kwa mujibu wa Taarifa kwa vymbo
vya habari iliyotolewa kwa wanahabari juzi na Naibu Msemaji wa Serikali
Zamaradi Kawawa alisema kuwa watapitia mkakati wa SADC wa uchumi wa
bahari na kutathmini maendeleo katika sekta za misitu wanyamapori na
utalii.
Alisema kuwa mkutano huo unakuja
baada ya serikali ya Tanzania kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo
kusini mwa Afrika inayojumuisha nchi 16 na Tanzania ndio mwenyekiti wa
jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka moja.
Alisema mkutano huo ni sehemu ya
majukumu ya uwenyekiti wa Nchi yetu chini ya mwenyekiti wake kwa sasa
Rais Dkta John Magufuli na kikao cha makatibu wakuu kitafunguliwa kesho
tareh 21 na Waziri wa maliasili na utalii Dkt Khamisi Kigwangallah ikiwa
ni sehemu ya kuandaa mapendekezo yatakayowasilishwa kwenye kikao cha
mawaziri.
Kikao cha mawaziri ambacho
kitafanyika tarehe 25 oktoba kwenye ukumbi huo huo wa AICC jijini Arusha
na utafunguliwa na makamu wa rais Samia Suluhu Hassan ambapo Tanzania
ni miongoni mwa wananchma wanaotekeleza mkakati wa SADC kuhusu usimamizi
wa sheria na vita dhidi ya Ujangili wa wanyamapori.
Aidha mkutano huo pia utajadili
masuala mbali mbali ya kuboresha mistu ikiwa ni pamoja na masuala ya
mazingira maliasili utalii na kubwa ni mabadiliko ya kimazingira na
ujangili unaovuka mipaka
No comments :
Post a Comment