
Makatibu Wakuu wa Wizara za
Maliasili,Utalii na Mazingira kutoka nchi za SADC wakiwa kwenye picha ya
pamoja baada ya kufungua mkutano huo

Katibu Mkuu wa Wizara ,Profesa
Adolfu Mkenda akifungua mkutano wa makatibu wakuu wa Wizara za
Maliasili,Utalii na Mazingira kutoka nchi za SADC.

Mkurugenzi wa idara ya Chakula ,kilimo na Maliasili kutoka Sektretarieti ya SADC ,Domingos Zephania Gove Akizungumza

washiriki wa mkutano
********************************
Makatibu
Wakuu kutoka Wizara za Maliasili,Utalii na Mazingira wa nchi za SADC
wameanza vikao vya kujadili na kuweka agenda za mkutano wa Mawaziri wa
sekta husika kutoka umoja huo ambapo wanatarajia kujadili mpango mkakati
wa pamoja wa kukabiliana na ujangili ili
kutomokeza ujangili katika
nchi mwanachama.
Katibu Mkuu wa
Wizara ,Profesa Adolfu Mkenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano
huo wa makatibu wakuu kutoka nchi mwanachama amesema kuwa mkutano huo
utajadili mambo mbalimbali ikiwemo vita dhidi ya ujangili ambayo
inapaswa kuungwa mkono kwa nchi zote mwanachama badala kuachwa kwa nchi
moja.
Mkenda amesema
kuwa nchi moja ni vigumu kupambana na ujangili hivyo tunahitaji
kuunganisha nguvu kwa nchi zote ili ziweze kufanikisha juhudi za
kupambana na ujangili.
“Tunahitaji kuwa
na mpango mkakati wa kukuza utalii katika nchi za SADC hii ni moja kati
ya ajenda muhimu zitakazojadiliwa” Alisema Profesa Mkenda
Mkurugenzi wa
idara ya Chakula ,kilimo na Maliasili kutoka Sektretarieti ya SADC
,Domingos Zephania Gove amesema kuwa wanahitaji kutembea pamoja kama
nchi za SADC katika kuweka mikakati katika masuala ya kimazingira,Utalii
na Wanyamapori .
Gove amesema kuwa wanahitaji kuthibitisha program za pamoja za kukuza utalii na kusimamia maliasili katika ukanda husika.
No comments :
Post a Comment