Wednesday, October 2, 2019

Mahakama ya Kimataifa yashindwa kutengua Hukumu ya aliyekuwa waziri wa mipango Rwanda



************************
Na Queen Lema Arusha
Aliyekuwa waziri wa mipango wa serikai ya mpito ya Rwanda  Bw. Augustine Ngirabatware ameshindwa kuwasilisha ushahidi wa kutosha wenye uwezo wa kuaminika katika kikao cha
rufaa cha mahakama ya kimataifa inayoshughulikia masalia ya makosa ya mauaji ya kimbari  ili kuweza kubatilisha  hukumu ya awali anayendelea kuitumikia.
Rais wa mahakama hiyo Jaji Theodor  Meron amesema kuwa  kupitia kifungu cha sheria namba 147 ya mwenendo wa ushuhuda Ngirabatware ambaye aliita mashahidi sita wameshindwa kutoa ushahidi wa ukweli unaounga mkono hoja  mpya ya kubatilisha ushahidi wa awali uliotolewa  kuwa sio wa kweli na hivyo hukumu ya awali bado inaendelea.
Mnamo Desemba 2012 mahakama ya mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR)ilimtia hatiani  Ngirabatware kwa kosa alilolifanya mwaka 1994 la kufanya  uchochezi wa moja kwa moja wa kufanya mauaji ya kimbari na makosa ya ubakaji na  kuhukumiwa miaka 35 jela  na baadae Desemba 2014 mahakama ya kesi za masalia ya makosa ya mauaji ya kimbari iliondoa kosa la ubakaji na kubaki na kifungo cha miaka 30.
Aidha  Julai 8 mwaka 2016  Ngirabatware  aliwasilisha ombi la kupitia upya hatia yake na Juni mwaka 2017 mahakama hiyo iliridhia  kusikiliza  kusikiliza shauri lake upya ambapo kesi hiyo ilianza kusikilizwa september 16 hadi 27 mwaka huu.

No comments :

Post a Comment