Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, ( CGF) Thobias Andengenye (aliyeshika bendera)
akiongoza msafara wa askari 11 wa jeshi hilo kupanda mlima Kilimanjaro.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye (kulia) akiongoza msafara
wa askari 11 wa jeshi hilo kupanda mlima Kilimanjaro.
**************************
KAMISHNA Jenerali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye amewaongoza
maofisa 11 wa jeshi hilo kupanda mlima Kilimanjaro kwa kuitaka jamii
kuwa wazalendo kwa kupenda utalii wa ndani na kutembelea hifadhi za
Taifa.
Akizungumza jana kamishna Jenerali Andengenye alisema watanzania wanapaswa kupenda vivutio vya utalii wa ndani.
Alisema askari
watapanda mlima Kilimanjaro kujionea ufahari uliopo ili kukuza uchumi wa
nchi wakiwawakilisha askari wa zimamoto wengine hapa nchini.
Alisema wenyewe
wanahusika na dharura zote za uokoaji isipokuwa za jinai ndiyo sababu
wakaonelea wapande juu ya Afrika kupitia mlima Kilimanjaro ambao ni
mrefu kwenye bara hilo.
“Sisi tunapaswa
tutumie karama tuliyopewa na Mungu kwa kutembelea na kujionea ili kukuza
uchumi wetu kwa watanzania wenyewe kuchangia pindi tukitembelea hifadhi
zetu,” alisema Andengenye.
Mkaguzi msaidizi wa
jeshi la zimamoto na uokoaji, Bilhah Chaila akizungumza wakati
wakijiandaa kupanda mlima Kilimanjaro aliwahamasisha wanawake wa ndani
na nje ya nchi kushiriki kwa wingi kwenye vivutio vya utalii.
Chaila alisema kuwa
wanawake wanauwezo mkubwa kama wanawake hivyo wanapaswa kushiriki
kuchangia pato la Taifa kwa kutembelea hifadhi za Taifa zilizopo sehemu
mbalimbali hapa nchini.
Kamishna Jenerali
Andengenye na maofisa hao 11 wanatarajia kupanda mlima Kilimanjaro na
kurejea ijumaa ijayo Octoba 4 mwaka huu.
Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu zaidi barani Afrika una urefu wa karibia mita 6,000 sawa na zaidi ya futi 20,000.
No comments :
Post a Comment