
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Dk.Leonard Akwilapo akizungumza jijini Dodoma leo
na Wandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya kuanzishwa kwa mitihani
ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili na Chuo kikuu cha Dar es
Salaam kuanzia Januari,mwaka 2020 katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya
Taaluma za Kiswahili, Prof.Aldin Kai Mutembei

Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma
za Kiswahili, Prof.Aldin Kai Mutembei,akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dodoma kuhusiana na kuanzishwa kwa mitihani ya Kimataifa ya
Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kuanzia
Januari,mwaka 2020

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini Bi.Sylvia Lupembe,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) mara baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia Dk.Leonard Akwilapo,kutangaza kwa Chuo Kikuu cha Dar Es
Salaam kuanzisha mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili
inayotarajia kuanza Januari,mwaka 2020
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
…………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Dk.Leonard Akwilapo,amesema
kuwa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM) kinatarajia kuanza kutoa Mitihani ya Kimataifa ya
Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili (MKUKi) kuanzia Januari mwaka 2020.
Hayo ameyasema leo jijni Dodoma wakati akitoa taarifa hiyo ya mitihani kwa waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano huo.
Dk.Akwilapo amesema kuwa hatua
hiyo ni jitihada za kuikuza na kuieneza Lugha ya Kiswahili ulimwenguni
kwa kuwa ni miongoni mwa lugha 10 zenye wazungumzaji wengi duniani.
” Lengo letu ni kuunga mkono
juhudi za Serikali za kukieneza Kiswahili na kusimamia ubora wake ambapo
sasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimechukua jukumu la kuanzisha
mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili sanifu ili lugha ya
kimataifa ipate nguvu zaidi hutungiwa mitihani ili wanaojifunza lugha
hizo waweze kutathminiwa na kupata vyeti,” Amesema Dk Akwilapo.
Dk.Akwilapo amesema kuwa mitihani
itafanyika mara sita kwa mwaka ikiendana na kipindi cha masomo ya
Kiswahili kwa kila ngazi na itafanyika kwa njia za kielektroniki katika
vyuo na vituo mbalimbali vya Kiswahili duniani.
“CKD(Udsm), kinakuwa ni Chuo Kikuu
cha kwanza duniani kutunga mitihani hii na kusimamia utahini na
usahihishaji wake na kutoa Cheti cha Kimataifa kinachoonesha kiwango cha
ujuzi wa mtahiniwa,”amesema Dk.Akwilapo
Hivyo Chuo kinabeba jukumu la
kuanzisha mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili sanifu na
ili lugha ya kimataifa ipate nguvu zaidi hutungiwa mitihani ili
wanaojifunza lugha hizo waweze kutathminiwa na kupata vyeti.
Ameeleza kuwa tayari kuna
makubaliano baina ya walimu wa Kiswahili wa CKD na walimu wanaofundisha
Kiswahili katika vyuo vya nje kuhusiana na mitihani hiyo ambayo itaanza
kutolewa mwakani.
“CKD imejiandaa kuhakikisha kuwa
mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iko madhubuti kuwezesha
mitihani hii kufanyika kwa ufanisi na kwa viwango vya kimataifa kwani
kuna wahitaji ambao watafanyia mitihani hii wakiwa katika nchi zao, sio
lzima wasafiri na kuja kufanyia mitihani yao hao Tanzania,”aliongeza
Aidha amefafanua kuwa walengwa wa
mitihani hiyo ni watu wote ambao wanajifunza Kiswahili kama lugha ya
pili au lugha ngeni katika ngazi mbalimbali ikilenga kupima usanifu
katika kusoma, kuandika, kuongea na kusiukichangia ambapo amesema
wanaamini wanapaswa kuongeza juhudi za kukuza Kiswahili ili kumuenzi
Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alifanya
jitihada kubwa za kueneza na kukuza lugha hiyo katika Nchi za Afrika na
duniani kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Prof.Aldin Kai Mutembei, amesema kuwa
mitihani hiyo itaitwa kwa jina la MKUKi.
Prof.Mutembei amesema kuwa kuna
wanafunzi wanasoma Kiswahili huko nje na walitamani kuja kwenye nchi
zinazozungumza Kiswahili lakini wangependa wawe na utambulisho kuwa
wanajua Kiswahili hawa ndio tunaowalenga.
No comments :
Post a Comment