
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara
wa TBL Group,Bruno akieleza ujumbe wa Balozi wa Japan jinsi kampuni
inavyoendesha shughuli zake.

Balozi wa Japan nchini na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL, Jemedari Waziri.

Meneja Usalama na Afya mahali pa
kazi wa TBL,Revocatus Rutakwa akieleza ujumbe wa balozi kuhusu kampuni
inavyozingatia usalama wakati wote.

Ujumbe wa Balozi wa japan nchini,ukifuatilia maelezo kutoka kwa wataalamu wa TBL wakati wa ziara hiyo.
……………………..
Balozi wa Japan nchini
Tanzania, Shinichi Goto,amefanya ziara katika kiwanda cha bia Tanzania
Breweries Limited (TBL), kilichopo Ilala, Dar es Salaam. Aliongozana na
ujumbe wa Maofisa wa ubalozi huo, ambapo waliweza kupata taarifa za
uwekezaji nchini, utendaji kazi wa
kampuni sambamba na kutembelea
kiwanda cha kutengeneza bia.
Katika ziara hiyo, Balozi Goto,
alipata maelezo ya jinsi kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya
kimataifa ya ABInBEV, inavyoendesha biashara zake sambamba na kuunga
mkono jitihada za serikali katika kufanikisha Malengo Endelevu ya Dunia
(SDGS’s).
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara
wa TBL Group, Bruno Zambrano, aliueleza ujumbe huo wa Balozi Guto,
jitihada zinazofanywa na kampuni kutekeleza masuala hayo kwa lengo
lakuifanya jamii kuwa na maisha bora na endelevu katika maeneo ya
kusaidia miradi ya maji salama, kuhamasisha matumizi mazuri ya maji,
utunzaji wa mazingira, kuwezesha wanawake kiuchumi, kutoa elimu ya
ujasiriamali sambamba na elimu ya unywaji wa kistaarabu, kuwezesha
wakulima wadogo wanaoiuzia kampuni malighafi na kutoa ajira nyingi kwa
wananchi wa Tanzania kupitia mtandao wa biashara zake.
Zambrano, pia alieleza kuwa
TBL imekuwa mstari wa mbele kuchangia pato la serikali kwa njia ya
kulipa kodi ambapo imeweza kutunukiwa tuzo ya Mlipa Kodi Bora nchini na
tuzo nyinginezo baadhi yake zikiwa tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora na
tuzo ya Mwajiri bora.
Balozi wa Japan nchini, Shinichi
Goto na ujumbe wake waliipongeza TBL kwa jitihada inazofanya kukuza
uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda sambamba na uwekezaji katika
teknolojia za kisasa na mifumo ya kisasa ya uendeshaji viwanda kwa
ufanisi wa kimataifa.
Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL,
Jemedari Waziri, alisema “TBL inawashukuru kwa ziara yenu hapa kiwandani
na kuweza kuona tulikiendelea na jitihada za kuchangia kukuza uchumi wa
Tanzania, kupitia uwekezaji wetu katika sekta ya viwanda na kilimo
sambamba na kulenga kunufaisha makundi mbalimbali katika jamii.
Tutaendelea kuongeza uwekezaji zaidi”.
Waziri, alisema kampuni imejipanga
kuhakikisha inafanya uwekezaji mkubwa wa matumizi wa teknolojia za
kisasa na kuwa na wataalamu ili kuhakikisha inazalisha bidhaa bora kwa
gharama nafuu ikiwa ni moja ya mkakati wa kufanikisha mkakati wa
serikali ya awamu ya tano wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
No comments :
Post a Comment