Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Vijana walioshiriki katika mafunzo
ya ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Green House)
katika Kijiji cha Ihemi alipotembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya
mafunzo hayo Mkoani Iringa.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Iringa Bi. Lucy Nyalu akieleza jambo kuhusu ushirikishwaji wa vijana
kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo walioshiriki katika mafunzo hayo.
Baadhi ya Vijana wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea
vijana hao kwa lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia
teknolojia ya kitalu nyumba.
Mratibu wa Mradi huo katika
Halmashauri ya Iringa Vijijini Bw. Daniel Mlay akitoa taarifa ya
utekelezaji wa mradi wa ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya Kitalu
Nyumba kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Holly Green Bw.
Octavian Laswai alipokuwa akikagua kitalu nyumba wakati wa ziara yake ya
kukagua maendeleo ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kupitia kitalu
nyumba, Mkoani Iringa.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Ihemi Bw. Antony Akata (wa pili kutoka kushoto) akimfafanulia
jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea eneo hiyo kwa
lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya
kitalu nyumba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Bi. Saada Mwaruka
alipokuwa akikagua chanzo cha maji yanayotumika kumwagilia Kitalu nyumba
hicho. (Katikati) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji
Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Venerose Mtenga.
******************
Na; Mwandishi Wetu
Programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu nyumba (Green house)
inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu imewapa
hamasa vijana kushiriki kwa wingi kwenye sekta ya kilimo
ikiwa ni chanzo cha kimoja wapo cha ajira nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Ziara yake ya kukagua
maendeleo ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kupitia teknolojia
ya Kitalu Nyumba, Mkoani Iringa.
Waziri Mhagama alieleza kuwa
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliamua kuanzisha programu hiyo
kwa lengo la kuwawezesha vijana kushiriki kwa wingi kwenye masuala ya
kilimo ili waweze kujiajiri wao wenyewe na kuajiri vijana wenzao kupitia
teknolojia hiyo.
“Mradi huu unatekelezwa kwenye
Halmashauri 185 nchini katika awamu hii ya kwanza ikiwa na lengo la
kuwawezesha vijana kuwa na ujuzi pamoja na stadi za kilimo cha kisasa
kupitia kitalu nyumba ambacho kina tija katika kuwapatia mazao bora na
mengi yatokanayo kwenye eneo dogo,” alieleza Mhagama
Alieleza kuwa Serikali imeendelea
kuwawezesha na kuwajengea uwezo vijana wa masuala ya ukuzaji ujuzi ili
waweze kuongeza tija kwenye shughuli wanazozifanya na zitakazo wakwamua
kiuchumi.
“Vijana wanaweza kupata ajira bora
katika kilimo endapo watawekewa mazingira bora kama kuimarisha
teknolojia na mbinu za kilimo,” alisema Mhagama.
Hata hivyo aliwasihii vijana
kuhakikisha wanatunza vitalu nyumba hivyo kwa kuwa watanufaika navyo na
vitawasaidia kufanilisha malengo yao sambamba na kuleta maendeleo
endelevu katika sekta ya kilimo.
Aidha alitoa wito kwa wakurugenzi
wa halmashauri zote nchini kuhakiksha wanawasilisha njia bora zaidi za
kuwapata vijana stadi zitakazo wajengea uwezo kupata teknolojia za
kisasa zitumikazo katika kilimo pamoja na kuwapatia mitaji ambayo
itawawezesha kujenga vitalu nyumba vyao binafsi.
Kwa Upande wake Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu
Bi. Venerose Mtenga alisema kuwa Ofisi hiyo inatekeleza programu
mbalimbali zitakazo wawezesha vijana kupata ujuzi na stadi stahiki
zitakazo wasaidia kuondokana na changamoto ya ajira.
Naye Mratibu wa Mradi huo katika
Halmashauri ya Iringa Vijijini Bw. Daniel Mlay alisema kuwa jumla ya
vitalu nyumba vinne vimejengwa na vijana 431 wameweza kunufaika na
mafunzo hayo.
“Tutaendelea kuwahamasisha vijana washiriki kwa kikamilifu katika mradi huu kwa kuwa una manufaa mazuri kwao,” alisema Mlay
Pia mmoja wa vijana walionufaika
kupitia Mradi huo Bw. Ramadhani Haule alieleza kuwa mradi huo wa Kitalu
Nyumba umewasaidia kupata elimu bora ya kilimo na umesaidia vijana
kuondoka kwenye makundi ya wasiokua na ajira.
“Tunaishukuru Serikali kwa
kutuamini na kutupatia ujuzi huu, tunaahidi tutaendelea kushirikiana
vijana wengi ili kujikwamua kiuchumi,” alisema
Katika ziara hiyo Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama alitembelea Vitalu Nyumba vilivyopo katika eneo la
Ihemi na Halmashauri ya Mafinga.
No comments :
Post a Comment