Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Iringa Mjini na Iringa
Vijijini pamoja na vionzi wa Vyama vya siasa na Viongozi wa Dini
kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa, Septemba 28, 2019.Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa
wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahnga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa
Halmashauri ya Iringa Mini na Iringa Vijijini pamoja na vionzi wa Vyama
vya siasa na Viongozi wa Dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa,
Septemba 28, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na
kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahnga.(Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametoa muda wa saa nne kwa Mkurugenzi wa Manispaa
ya Iringa Himid Njovu awe ameandika barua ya kusitisha ujenzi wa ukumbi
wa mikutano na sherehe katika eneo la shule ya msingi Gangilonga.
Amesema maeneo yote ya taasisi za
elimu nchini hayaruhusiwi kujengwa miradi ambayo
haihusiani na masuala
ya elimu, hivyo amtaka mkurugenzi huyo kusitisha mkataba na mtu
aliyemkodisha eneo hilo na kisha alizungushie uzio kwa matumizi ya
shule.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo
(Jumamosi, Septemba 28, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa
Halmashauri ya wilaya ya Iringa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na
Madiwani wa Halmashauri hizo akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya
kikazi mkoani Iringa.
“Mkurugenzi kafute mikata yote ya
ujenzi wa miradi katika eneo la shule ya Gangilonga pamoja na shule ya
Wilolesi kwa sababu maeneo hayo hayaruhusiwi kujengwa miradi
isiyohusiana na elimu. Eneo hilo lisafishwe na ujengwe uzio.”
Kwa upande wake, Mwanasheria wa
Manispaa ya Iringa Nocholous Mwasungura amesema aliandaa mkataba wa
kupangisha eneo kwa maelekezo ya Kamati ya Fedha, ambapo Waziri Mkuu
alimuuliza kwa nini hakuwashauri kuhusu suala hilo kwa sababu tayari
Serikali ilishatoa waraka wa kuzuia jambo hilo.
Pia, Waziri Mkuu amemwagiza Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Ally Happi ofisi ya ardhi ya Manispaa ya Iringa
kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka wananchi juu ya Afisa
Ardhi ambaye anadaiwa kujigawia viwanja vingi pamoja na kugawa kiwanja
kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Ally Happi aliwaonya watumishi hao kutojihusisha na vitendo vya rushwa
na matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kuacha chuki, ubinafsi na roho
mbaya na badala yake washikamane na wafanye kazi wa bidii.
Naye,Mkuu wa wilaya ya Iringa,
Richard Kasesera aliiomba Serikali izisaidie halmashauri za wilaya hiyo
vyombo vya usafiri kwa sababu magari mengi ni chakavu hali
inayosababisha Mkurugenzi wa Manispaa awe anaomba lifti kwake. Waziri
Mkuu amewataka waombe kibali cha ununuzi wa magari na watumie fedha zao
za ndani.
No comments :
Post a Comment