Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akiangalia mkanda wa ubingwa wa dunia wa ngumi za kulipwa waWBO
aliokabidhiwa Bondia Mtanzania, Abdallah Shaban aka Dullah Mbabe
alipotembelea Bungeni leo tarehe 4 Septemba 2019 jijini Dodoma. Bondia
huyo ameibuka mshindi wa Dunia katika mchezo wa ngumi za kulipwa na
kushinda mkanda huo katika pambano la uzito wa kilo 76 dhidi ya Bondia
kutoka China pambano lililochezwa nchini humo hivi karibuni. Kulia ni
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza na Rais wa Kamisheni ya
Ngumi za Kulipwa Tanzania, Joe Anea (wapili kushoto).
Mbunge
wa Kuteuliwa, Mhe. Salma Kikwete(katikati) na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia)
wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamisheni ya Ngumi Tanzania
na Mabondia walioshinda mapambano ya kimataifa walipotembelea Bungeni
leo tarehe 4 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mabondia hao kulia ni Abdallah
Shaban aka Dulla Mbabe bingwa wa dunia aliyeshinda mkanda wa WBO, Maono
Ally aliyeshinda mkanda wa WBC na Bruno Tarimo aka Vifua viwili
aliyeshinda mkanda mkanda wa IBF Intertional.
Pages
Wednesday, September 4, 2019
MABONDIA WAWA KIVUTIO BUNGENI LEO
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment