
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Dkt. Augustine Mahiga amepokea Mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya
Mirathi na Sheria ya Ndoa yaliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe. Paul Makonda Ofisini kwake katika mji wa Serikali Mtumba
jijini Dodoma.
Mhe. Makonda amewasilisha
mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya hizo kwa Mhe. Dkt Mahiga ili
zifanyiwe marekebisho na kuendana na wakati na zitoe haki kwa wanawake
nchini
pindi Mume anapofariki na hivyo kuwaondolea mateso na manyanyaso
Wajane nchini.
Akizungumza baada ya kupokea
mapendekezo hayo Mhe. Mahiga amemuahidi Mhe. Mkuu wa Mkoa ambaye
aliambatana na viongozi wa Chama cha Wajane Tanzania kuwa Wizara
itayapitia mapendekezo yao na kuyafanyia kazi stahiki.
“Niwashukuru kwa kazi hii kubwa
mliofanya ambayo Mhe. Mkuu wa Mkoa umenikabidhi leo hii, hii ni ishara
ya kazi kubwa na nzuri unayoifanya kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam,
nikuahidi wewe na timu yako kwamba mimi na timu ya wataalamu wangu
tutayapitia mapendekezo yenu na kuyafanyia kazi ili tuweze kwenda na
wakati na kutoa haki kwa wananchi wetu,” alisema Mhe. Waziri
Amesema Wizara ya Katiba na Sheria
itahakikisha inalifanyia kazi suala hilo hasa ikizingatiwa kuwa utafiti
huo umefanywa katika mkoa wa Dar es Salaam ambao una uwakilishi wa watu
kutoka mikoa yote nchini na kuongeza kuwa haki nyingi za wanawake
zimekuwa zinadaiwa lakini suala la mirathi ni kama limesahauliwa.
Awali akikabidhi taarifa hiyo Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam alisema Sheria ya Mirathi ya Mwaka 1865 ,
Sheria ya Mirathi ya Kimila ya Mwaka 1963 na Sheria ya Mirathi ya Kidini
ya Mwaka 1963 zimeonekana kuwa na Mapungufu makubwa na zimepitwa na
wakati na kutokana na hali hiyo zinawakandamiza wanawake na
kuwanyanyasa.
Ametaja vipengele wanavyopendekeza
kufanyiwa marekebisho kuwa ni pamoja na kumpa uhalali Mke wa marehemu
kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, mjane kupewa haki ya
kurithi na kusimamia mali za marehemuutafiti kutoondolewa kwenye nyumba,
Mali kuhamishwa, Usawa wa watoto katika kumiliki mali za marehemu bila
kujali jinsia pamoja na haki ya mtoto wa nje ya Ndoa, Mjane kutoondolewa
kwenye nyumba.
Vifungu vingine ambavyo Mkuu wa
Mkoa ameeleza kuwa ni kandambizi kwa Mjane ni pamoja na kile
kinachoruhusu Mjane kurithiwa na kile kinachomnyima Mwanamke haki ya
kurithi ardhi ya ukoo.
Amesema utafiti waliMjane
kutoondolewa na Kongamano la Wajane zaidi ya 5,181 aliokutana nao mwezi
April ambapo alipokea Kero na Malalamiko mbalimbali kutoka kwa Wajane
waliohudhuria kongamano hilo na kuamua kuunda kamati iliyoshirikisha
Wadau na Wataalamu mbalimbali kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia ambao
waliopitia malalamiko hayo na kuja na mapendekezo hayo.
Akizungumza katika kikao hicho
Mwenyekiti wa Chama cha Wajane Tanzania Bi Rose Sarwat ameishukuru
Wizara kwa kukubali kupokea mapendekezo hayo ili kuyaangalia na kuja na
marekebisho ambayo yatawafanya wajane nchini kuishi kwa amani na upendo
baada ya kufiwa na waume zao.
No comments :
Post a Comment