Monday, September 30, 2019

BENKI YA BIASHARA MKOMBOZI YAZINDULIWA RASMI NJOMBE




NJOMBE
Kufuatia taasisi nyingi za fedha kukwepa kutoa mikopo katika sekta ya kilimo , wakazi wa mkoa wa Njombe wametumia fursa ya uzinduzi  wa tawi la benki ya Mkombozi mkoani humo kuishauri taasisi hiyo kujikita zaidi kwa wakulima , wafugaji na wafanyabishara ili kuleta tija kwa wakazi ambao wanasifika kwa uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula.
Benki ya Mkombozi imezindua tawi la 11 katika mkoa wa Njombe na kupata mapokeo makubwa kwa wakazi wa mkoa huo baada ya kujipambanua katika kuwahudumia zaidi wakulima huku ikiwa na lengo la kufanya mapinduzi katika sekta ya biashara , ufugaji na kilimo.

Angela Mwangeni na Benard Mlyuka ambaye ni mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Njombe wanasema ujio wa taasisi hiyo ya fedha utaongeza mzunguko wa fedha mtaani huku pia wakitoa ushauri juu ya kupunguzamasharti ya kuwakopesha wakulima.
Awali mkurugenzi wa benki ya biashara ya Mkombozi Tanzania Thomas Enock ameweka bayana mkakati wa taasisi hiyo ya fedha ambapo amesema kwanza ni kuleta mapinduzi katika sekta ya muhimu tatu ambazo ni kilimo, ufugaji na biashara ili kufikia uchumi wa viwanda unaokusudiwa na serikali ya Tanzania.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka pamoja na spika mstaafu wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Anne Makinda wamesema benki imekuja wakati muafaka kwasababu mkoa huo unawakulima wengi ambao wanahitaji kuwezeshwa mikopo yenye masharti nahafuu ili kutanua wigo wa shghuli zao.

Uzinduzi wa taasisi hiyo mkoani Njombe unafikisha idadi ya matawi 11 kote nchini ambayo yamefunguliwa katika kipindi cha miaka 10 tangu kuanza kwake.

No comments :

Post a Comment