
Meneja wa benki BancABC Tanzania
Kanda ya Dar es Salaam Ferdinand Mgeni (aliyesimama) akiongea wakati wa
kukabidhi rambi rambi ya Tzs500,000/- kwa mke wa mmoja ya mteja wa Mkopo
Rahisi ambaye alifariki kwenye tukio lilofanyika jana (leo) jijini Dar
es Salaam. Mkopo Rahisi ni mkopo ambao utolewa na BancABC ambapo mteja
anapofariki benki hiyo ufuta deni la mkopo pamoja na kutoa rambi rambi
ya Tzs500,000/- kwa familia ya marehemu.

Meneja wa benki ya BancABC
Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Ferdinand Mgeni akikabidhi hundi ya
Tzs500,000/- kwa Maria Privatus ambaye ni mkazi wa jijini Dar es Salaam
baada ya kufiwa na mume wake. BancABC Tanzania kupitia Mkopo Rahisi
ufuta deni la mkopo pamoja na kutoa pole kwa familia ya mteja wake pale
anapofariki akiwa na na Mkopo Rahisi kutoka benki hiyo. Anayeangalia ni
Ofisa Mikopo wa benki hiyo Ally Bendera.

Mnufaika wa Mkopo Rahisi Maria
Privatus akionyesha hundi baada kukabidhiwa na BancABC leo jijini Dar es
Salaam. Mkopo Rahisi ni mkopo ambao utolewa na BancABC ambapo mteja
anapofariki benki hiyo ufuta deni la mkopo pamoja na kutoa rambi rambi
ya Tzs500,000/- kwa familia ya marehemu
…………………….
Benki
ya BancABC ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara Tanzania imetoa msaada
wa mazishi kwa Mke wa mmoja wa wateja wake wa Mkopo Rahisi wa jijini
Dar es Salaam ambaye hivi karibuni alifiwa na mume wake. Mkopo Rahisi ni
moja ya huduma ambayo hutolewa na BancABC kwa ajili ya kufariji familia
ya mteja wake inapotokea kifo kwa kufuta mkopo uliokuwa umebaki pamoja
na kutoa msaada wa Tzs500,000/- kwa familia.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi hundi ya fedha hizo kwa
Maria Privatus ambaye mume wake alikuwa ni mteja wa BancABC Mkopo Rahisi
kabla ya kufariki, Meneja wa BancABC Kanda ya Dar es Salaam Ferdinand
Mgeni alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikitoa msaada kwa familia ambayo
mteja alikuwa na Mkopo Rahisi kutoka BancABC. ‘Kile ambacho mnaona
tukifanya hapa leo ni jambo ambalo tulikuwa tukifanya siku zote. Sisi
BancABC ambao ni kampuni tanzu ya Atlas Mara Tanzania tuliamua kuwa na
kipengele cha aina hii kwenye mikopo yetu ya Mkopo Rahisi ili tuwe
tofauti na wengine kwenye soko. Lakini zaidi ni kufanya familia ya
wafiwa kuwa na amani kwani mbali na kutoa rambi rambi ra Tzs500,000/-
lakini pia tunafuta deni la mkopo ambao marehemu alikuwa anadaiwa, Mgeni
aliongeza.
Mgeni
aliongeza kuwa mkopo wa Mkopo Rahisi unao faida nyingi kwa mteja kwani
una riba ya chini kwa mwezi. Nia yetu ni kupunguza mzigo kwa wateja
wakati wa kulipa mikopo yao. Vile vile Mkopo Rahisi unatoa muda mrefu wa
kulipa kwani muda wake ni miezi 72 (miaka 6) na wateja anaweza kupata
mkopo hadi TZS40 milioni.
Naomba
nichukue fursa hii kuwaomba Watanzania kutembelea tawi lolote la
BancABC na kupata mkopo wa Mkopo Rahisi ambao ni rahisi na haraka
kupata. Wateja wetu wanao uhuru wa kutumia mkopo kwa uhuru wao iwe ni
kulipa ada ya shule, kodi ya nyumba na mengineo lakini pia muda wowote
mteja anaweza akiongezea kuchukua mkopo wake.
Akizungumza
baada ya kupokea rambi rambi hiyo ya Tzs500,000/-, Maria Privatus
ambaye mume alifariki akiwa ni mwalimu wa shule ya wasichana ya Zanaki
ya jijini Dar es Salaam alisema, ‘Nawashukuru sana BancaABC kwa kutoa
muda wenu na kuja kunitembelea pamoja na kunipa rambi rambi hii.
Nimekuwa nikifanya biashara ya kuuza chakula hapa shuleni ambapo mume
wangu alikuwa ni mwalimu. Nitatumia pesa hii kwa ajili ya kukuza
biashara yangu na hatimaye niweze kuendesha familia kwani kwa sasa
nimebaki bila ya kuwa na mtu wa kunisaidia.
Maria
aliongeza, kwa sasa mimi nishahidi mzuri wa BancABC. Wakati kutangaza
kwamba mteja wenu wa Mkopo Rahisi anapofariki, benki mara moja ufuta
deni la mkopo wake pamoja na kusaidia familia ya marehemu kwa kiasi cha
Tzs500,000/- sikuamini mpaka haya ya kwangu yalipotokea. Nitaendelea
kuwa mteja wenu na nawaomba Watanzania wajiunge na BancABC kwani ni
benki yenye bidhaa na huduma za uhakika kwa hapa nchini.
No comments :
Post a Comment