Sunday, August 18, 2019

WAFANYAKAZI WA TANESCO WACHANGIA DAMU HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI (MNH)

NA K-VIS BLOG
WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Kanda ya Dar es Salaam na Pwani wakiongozwa na Meneja Mwandamizi wa Kanda hiyo, Mhandisi Hassan Said, leo Agosti 16, 2019 wamefika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kitengo cha Damu Salama na kuchangia damu ili kuwasaidia majeruhi wa ajali ya moto wa gari la mafuta Morohgoro lakini na wale wenye uhitaji wa damu na hawana jamaa wa kuwasaidia.
Utaratibu wa wafanyakazi wa TANESCO kujitolea damu ni wakawaida ambapo mwkaa jana walijitolea damu kwenye hospitali ya Tumbi Kibaha Mkoani Pwani.
Kanda ya Dar es Salaam na Pwani inaundwa na Mikoa ya TANESCO Kinondoni Kaskazini, kinondoni Kusini, Temeke, Ilala na Mkoa wa Pwani.
 Meneja Mwandamizi wa Kanda hiyo, Mhandisi Hassan Said, akijiandaa kwa zoezi hilo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam leo Agosti 16, 2019.








No comments :

Post a Comment