Na Anthony Ishengoma WAMJW
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile amesema kuwa mtoto wa kike uzidi kukua kiuchumi
kulingana na muda anaokaa shuleni akiongeza kuwa mwanamke anavyozidi
kujiendeleza kielimu upunguza uwezekano wa kuwa na idadi kubwa ya watoto
na na kufanyiwa vitendo vya kikatili.
Dkt.
Ndugulile amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa akiitambulisha
Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake
na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja inayolenga kushirikisha wanaume na wanawake kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kupitia mbinu anwai.
Aidha
Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa kuwepo kwa elimu bure nchini kwa kiasi
kikubwa kumepunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ikiwemo mimba
na ndoa za utotoni pamoja na uwepo wa Sheria inayotoa adhabu ya kifungo
cha miaka 30 jela kwa anayebainika kufanya vitendo hivyo.
Dkt.
Ndugulile ametaja wastani wa watoto kwa mwanamke wa Tanzania kuwa
watano hivyo kadri msichana anavyokaa shuleni anapunguza uwezekano wa wa
kuzaa watoto wengi lakini pia akasema uwezi ukalinganisha kipato cha
Msichana wa kidato cha nne na yule wa Darasa la Saba.
Akizungumzia
kuhusu kauli mbiu ya kampeni hiyo Dkt. Ndugulile ameviambia vyombo vya
habari kuwa yeye kama Naibu Waziri anachukizwa na vitendo vya ukatili
dhidi ya Wanawake hivyo akachukua fursa hiyo kuhamasisha pia wanaume
wengine nchini kuchukia vitendo hivyo akiitaja kauli mbiu ya Kampeni
hiyo kuwa ni ''Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi’’.
Akizungumzia
hali ya ukatili wa kijinsia Nchini Dkt. Ndugulile amesema taarifa ya
hali ya Uhalifu nchini ya Mwaka 2017 inaonesha kuwa jumla ya watu
41,416 waliofanyiwa ukatili wa kijinsia walitoa taarifa kwenye vituo vya
polisi ikilinganishwa na watu 31,996 waliofanya hivyo mwaka 2016.
Dkt.
Ndugulile ameyataja baadhi ya matukio ya ukatili yaliyotolewa taarifa
kuwa ni ubakaji, vipigo, matusi, ulawiti, kutupa watoto, ukeketaji na
kuwapa mimba wanafunzi na kuongeza kuwa kati ya mataukio hayo 41,416
yaliyotolewa taarifa mwaka 2017 matukio 27,703 sawa na asilimia 67
yalifanywa dhidi ya wanawake na watoto.
Dkt.
Ndugulile ameongeza kuwa asilimia 40 ya wanawake wa umri kati ya miaka
15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili au kingono mara moja au zaidi
katika kipindi hicho cha maisha wakati wanawake asilimia 20 wenye umri
miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili katika kipindi cha miezi 12
iliyopita.
Dkt.
Ndugulile amefafanua kuwa Wizara ianshirikiana na wasanii katika
kufikisha ujumbe na amemtaja Msanii Nurdin Bilal Maarufu SHETTA kuwa
amejitolea kuwa Balozi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto na
atataumia jukwaa la Sanaa kuelimisha jamii kwa kutumia mziki wake na
mitandao ya kijamii.
''Ni
matarajio yangu kwamba kampeni hii ya Kupinga Ukatilili wa Kijinsia
Kitaifa italeta mabadiliko makubwa kupitia jumbe mbalimbali
zilizoandaliwa kupitia muziki, machapisho, nyimbo, shuhuda na Semina
zitakazokuwa zinaendelea kutolewa kwenye majukwaa mbalimbali kipindi cha
kampeni’’. Alihitimisha Dkt. Ndugulile.
No comments :
Post a Comment