Meneja
wa TANESCO Mkoani Simiyu Bi. Rehema Mashinji (katikati), akitoa elimu ya
matumizi bora na sahihi ya umeme kwa wananchi (hawapo pichani)
waliotembelea banda la TANESCO kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya
Nyakabindi, nje kidoko ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu Agosti 4, 2019.
Wananchi wakielimishwa kuhusu shughuli za TANESCO lakini pia matumizi sahihi na yaliyo bora ya umeme
Bi. Mashinji (kushoto), akimsikiliza mwananchi huyu aliyekuwa kitaka ufafanuzi kuhusu masuala ya umeme.
Wananchi wakiwa na vipeperushi vyenye maelezo ya kina kuhusu shughuli za TANESCO lakini pia matumizi bora na sahihi ya umeme.
Mtaalamu
wa TANESCO (kulia), akitoa elimu kwa Mzee Mtaka, baba wa Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, ambaye alitembelea banda la Shirika hilo
kujielimisha kuhusu masuala ya umeme Agosti 4, 2019.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
SHIRIKA
la Umeme Nchini TANESCO mkoani Simiyu, limesema kumekuwepo na mwamko mkubwa wa
wananchi wa mkoa huo kutumia umeme kama kichocheo cha upanuzi wa shughhuli zao
za kiuchumi.
Meneja
wa TANESCO Mkoani Simiyu, Mhandisi, Rehema Mashinji ameyasema hayo leo Agosti 4, 2019 katika maonesho ya
Nanenane viwanja vya Nyakabindi mkoani humo kuwa, kuboreka
kwa hali ya umeme kumeleta msukumo mpya ambapo wananchi wameanzisha mashamba makubwa ya
umwagiliaji ambapo pampu za kusukuma maji zinatumia umeme.
Alitoa
mfano kuwa yupo mwekezaji mmoja mzawa wilayani humo ambaye anaendesha kilimo
kikubwa cha umwagiliaji, TANESCO imemuwekea umeme wa kutosha kuhudumia mashamba
yake.
“Sisi
TANESCO mkoani Simiyu tuko vizuri, tumewezesha wananchi wengi kuanzisha
mashamba makubwa ya kilimo cha umwagiliaji huko Busega ambao wanalima mwaka
mzima, upande wa ufugaji tumewezesha kuanzishwa kwa viwanda vya kusindika
maziwa na kuhusu uvuvi tumepeleka umeme kwenye soko kuu la Ramadi na wananchi wanauza samaki na kufanya kazi
masaa 24 kila siku tumewapelekea huduma ya umeme na wameweka taa.” Alifafanua Mhandisi Mashinji.
Alisema
Simiyu ni wakulima wakubwa wa pamba, na tayari mkoa unatarajia kuanzisha
kiwanda cha kutengeneza vifaa tiba kupitia pamba, na sisi kama Shirika tuko
tayari kuwapelekea umeme pindi mipango ya kuanzisha kiwanda hicho
itakapokamilika.
“Tunategemea
kuanzishwa kwa viwanda vingi Zaidi vya kutengeneza vifaa tiba huko Dutwa hapa Simiyu.”
Alifafanua.
Mhandisi Mashinji amemshukuru Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani kwa kutoa punguzo
kubwa kwa wananchi ambapo wananachi wakitaka kuunganisha umeme hususan vijijini gharama ni Shilingi elfu 27,000/= tu.
“Wananchi
wengi waombe umeme ili tuwaunganishie, na kwabahati nzuri Simiyu umeme
umetawanyika kila kona na nia yetu umeme umfikie kila mwananchi hadi wa pembezoni.”
Alisisitiza Meneja huyo wa TANESCO mkoani Simiyu.
Aidha
alisema, wataalamu wa TANESCO waliopo katika maonesho ya Nanenane hapa
Nyakabindi hivi sasa, wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi bora na
sahihi ya umeme, lakini pia jinsi ya kutunza miundombinu ya umeme na
wawe mabalozi wa Shirika dhidi ya wahalifu wa miundombinu ya umeme
kwenye maeneo yao kwa kutoa taarifa pindi wanapohisi kuna uhalifu
unataka kufanyika.
No comments :
Post a Comment