Thursday, August 8, 2019

TAGCO YAWAPONGEZA MAAFISA HABARI WA SERIKALI KWA KUTEKELEZA WAJIBU WAO VEMA MAONESHO YA NANENANE NYAKABINDI, SIMIYU

 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Maafisa Habari wa Serikali (TAGCO), Bi. Sarah Msika (kulia), akisalimiana na Meneja Mkuu wa TAZARA upande wa Tanzania Bw. Fuad Abdallah (kushoto), huku Afisa Uhusiano wa TAZARA-Tanzania, Bi.Regina Tarimo (katika) na mjumbe wa TAGCO,Bi.Gaudensia Simwanza (wapili kulia), wakishuhudia wakati Bi. Msika alipokuwa akiwatembelea maafisa habari wa Serikali kwenye mabanda mbalimbali ya taasisi wanazofanyia kazi kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa Mkoani Simiyu.
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Sebera Fulgence (kushoto), akifafanua jambo kwa Makamu Mwenyekiti wa TAGCO Bi. Sarah Msika alipotembelea banda la Mfuko huo viwanja vya Nanenane Mkoani Simiyu.
 Afisa Uhusiano wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, (TAEC)Bi. Angela Msangi (kulia), akizungumza na Bi. Msika kwenye banda la Tume hiyo viwanja vya Nanenane Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Meneja Uhusiano wa TTCL, Bw. Nicodemus Mushi (kulia), akiwa ametembelewa na Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sara Msika (wapili kushoto) na mjumbe wa Chama hicho, Bi. Gaudensia Simwanza kwenye banda la TTCL viwanja vya Nakabindi kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa Mkoani Simiyu. 
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MAAFISA habari wa Serikali wamepongezwa kwa kazi nzuri wakati wakitekeleza majukumu yao katika kipindi cha maonesho ya Nanenane kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Maafisa Habari wa Serikali (TAGCO), Bi. Sarah Msika wakati alipokuwa akiwatembelea Maafisa hao kwenye mabanda mbalimbali ya taasisi za Serikali zilizoshiriki maonesho hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya pili mfululizo kwenye viwanja hivyo.
“Kwanza kabisa napenda niwapongeze maafisa habari wa Serikali ambao wako hapa kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu kwenye maonesho ya Nanenane kwa kuziwakilisha vema taasisi zao kwa kufafanua shughuli mbalimbali za Taasisi hizo za Umma zinavyowahudumia wananchi.” Alisema Bi. Msika.
Pia alisema amefurahishwa na mwamko wa maafisa habari hao wa Serikali ambao wengi wamejiunga na TAGCO ambayo lengo lake ni kuwaleta pamoja Mafisa hao kwa lengo la kubadilishana uzoefu katuka kuhakikisha taarifa za shughuli za serikali zinawafikia wananchi kwa usahihi na kwa muda muafaka.
Maonesho ya Nanenane yanafikia kilele Alhamisi Agosti 8, 2019 ambapo licha ya kufanyika kitaifa Mkoani Simiyu, pia yalifanyika katika kanda tatu za Kaskazini ambapo yalifanyika jijini Arusha, Kanda ya Mashariki yalifanyika Mkoani Morogoro na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yalifanyika jijini Mbeya.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi.

No comments :

Post a Comment