Serikali
kupitia Wizara ya Kilimo imezindua rasmi mpango wa Bima ya mazao
mbalimbali ambao utaanza na wakulima wa zao la pamba Mkoa wa Simiyu na
kahawa katika Mkoa wa Kagera.
Mpango
huo umezunduliwa leo na Waziri wa kilimo Japhet Hasunga katika viwanja
vya Nyakabindi Mkoani Simiyu yanakoendelea maonyesho ya sikuu ya
wakulima kitaifa (Nanenane).
Akizungumzia
bima hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Dk.
Elirehema Doriye, amesema wakiwa kama watekelezaji wa mpango huo
watahakikisha wakulima wote nchini wanapatiwa bima ya mazao yao.
Kwa
upande wake Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, ameitaka NIC kuhakikisha
wakulima wote wa mazao makuu matano wanajiunga na bima hiyo ili kuweza
kubadilisha kilimo kuwa cha kisasa zaidi na chenye tija.

No comments :
Post a Comment