Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Augustine Mahiga,akizungumza
wakati wa kufungua kikao cha Mawaziri, Makatibu wakuu wa Wizara na wakuu
wa taasisi zinazounda jukwaa la haki jinai ambao ulikuwa wa kujadili
hitimisho la mchakato wa sekta ndogo ya mfumo wa haki za jinai,zoezi la
majadiliano yaliyoanza Julai mwaka huu.
Katibu wa Wizara ya
Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome,akizungumza katika kikao cha
kujadili hitimisho la mchakato wa sekta ndogo ya mfumo wa haki za
jinai,zoezi la majadiliano yaliyoanza Julai mwaka huu.
Kamishna wa polisi
mstaafu Laurean Tibasana.akitoa taarifa katika kikao cha kujadili
hitimisho la mchakato wa sekta ndogo ya mfumo wa haki za jinai,zoezi la
majadiliano huo ambao ulianza Julai mwaka huu.
Sehemu ya wadau
wakifatilia kikao cha kujadili hitimisho la mchakato wa sekta ndogo ya
mfumo wa haki za jinai,zoezi la majadiliano huo ulioanza Julai mwaka
huu.
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Augustine Mahiga,akiwa katika
picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha Mawaziri, Makatibu
wakuu wa Wizara na wakuu wa taasisi zinazounda jukwaa la haki jinai
jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Augustine Mahiga,amesema kuwa Serikali inakuja na
mkakati wa miaka mitano utakaotekelezwa na Wizara na taasisi mbalimbali katika maeneo yanayohitaji mfumo wa maboresho ya haki jinai hapa nchini.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Augustine Mahiga,amesema kuwa Serikali inakuja na
mkakati wa miaka mitano utakaotekelezwa na Wizara na taasisi mbalimbali katika maeneo yanayohitaji mfumo wa maboresho ya haki jinai hapa nchini.
Dk.Mahiga ameyasema leo jijini Dodoma wakati
akifungua kikao cha Mawaziri, Makatibu wakuu wa Wizara na wakuu wa
taasisi zinazounda jukwaa la haki jinai.
Mkutano huo wa kujadili hitimisho la mchakato wa
sekta ndogo ya mfumo wa haki za jinai,zoezi la majadiliano likianza
Julai mwaka huu.
Dk. Mahiga amesema kuwa mara ya mwisho kupitia
mfumo huo na kuufanyia maboresho ni takribani miaka 20 hivyo ni muhimu
kupitia ili kuendana na wakati tuliona nao sasa.
Hata hivyo amesema kuwa baada ya mapitio ya
mfumo huo yatapitishwa na kujadili maeneo yaliyopendekezwa kuboreshwa
ili kufanya mfumo huo kuwa Rafiki kwa wadau wote wa haki jinai.
” Niwapongeze wataalamu wetu ambao mmekua hapa
kwa kwa kipindi cha miezi miwili na wote ambao mmeshiriki katika kazi
hii hadi hatua hii ya leo.
Dk.Mahiga amesema kuwa mfumo huo unahusisha
mnyororo wa hatua mbalimbali zinazotolewa wakati wa kushughulikia
uhalifu wa kuanzia katika ngazi ya kuzuia uhalifu kufuatilia mienendo
yao wanapomaliza kutumikia adhabu.
Waziri amesisitiza zaidi kuwa katika mnyonyoro
huo mambo mbalimbali yamewekwa kisheria ya namna ya kushughulika na
wahalifu ambayo yanashughulikiwa na Vyombo au taasisi za jukwaa la haki
jinai hivyo lazima kufanya maboresho
Naye Katibu wa Wizara
ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome amesema kuwa kikao hiko ni
muhimu sana kwa sababu kina lenga kufanya majadiliano ya hitimisho la
mchakato wa maboresho ya sekta ndogo ya mfumo wa haki jinai.
Hata hivyo amesema
kuwa ni vema nao wataalamu waliopo wanatumia nafasi hiyo kujadili
maboresho hayo ili yalete tija na jamii kwa ujumla.
Prof.Mchome amesema kuwa kutokana na hilo wanapaswa kutumia nafasi hiyo kutekeleza kile kinachotakiwa ndani ya majadiliano hayo.
Naye Kamishna wa
polisi mstaafu Laurean Tibasana amesema kuwa wanaipongeza serikali
kutokana na jitihada inazofanya katika maboresho ya sekta ndogo ya
sheria ya mfumo wa haki jinai.
Aidha amesema kuwa
hilo litasaidia nchi kuwa na maendeleo kutokana na kwamba kutasaidia
kupunguza uhalifu mbalimbali ikiwemo kurekebisha tabia za wahalifu na
kufuatilia mienendo yao wanapokuwa wamemaliza kutumikia adhabu
walizopewa.
No comments :
Post a Comment