Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua
mkutano na wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka katika
ukumbi wa kimataifa wa mikutano JNICC Jijini Dar es salaam leo tarehe 29
Agosti 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu
ya washiriki wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe
Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na
wasindikaji wa mazao ya nafaka katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano
JNICC Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Agosti 2019. (Picha Zote Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumzia fursa zilizopo katika
tasnia ya nafaka wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na
wasindikaji wa mazao ya nafaka katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano
JNICC Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Agosti 2019. (Picha Zote Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Dar es salaam
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 29 Agosti 2019
wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka
katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano JNICC Jijini Dar es salaam na kuongeza
kuwa, Serikali peke yake, haiwezi kuziondoa changamoto hizo bila wafanyabiashara,
wasindikaji na wasafirishaji kushirikiana na Serikali.
Katika
mkutano huo waziri Hasunga amezitaja fursa zilizopo kwenye tasnia ya Nafaka
kama ambazo ni pamoja na eneo linalofaa kwa kilimo ambalo linakadiriwa kuwa hekta
milioni 44. Kati ya hizo, hekta milioni 29.4 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Eneo hilo, linafaa kwa kilimo cha mazao yote ya biashara na chakula, yakiwemo
mazao ya nafaka kama mahindi, mtama, mpunga, ngano na mengineyo.
Fursa
nyingine alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati, inajitahidi sana
kufikisha umeme vijijini ambako ndiko nafaka zinapatikana. Hadi sasa asilimia
70 ya vijiji nchini, vimepatiwa umeme. Umeme huo unatakiwa utumike pia katika
eneo la usindikaji. Hadi sasa, sehemu ndogo ya maghala kwenye usindikaji wa
mpunga na mahindi kupitia mashine za kukoboa mpunga na mahindi.
Mhe
Hasunga alisema kuwa Kuna baadhi ya maeneo, maghala mazuri yamejengwa kwa usimamizi wa Serikali ili kuwa na uhifadhi
mzuri wa nafaka. Mfano, maghala mengi yaliyojengwa wakati wa BRN bado
hayajaweza kutumika ipasavyo.
Alisema
Nchi yetu ina ikolojia tofauti tofauti, hali hii inasababisha baadhi ya maeneo
kuwa na mvua za kutosha, na maeneo mengine kuwa na uhaba wa mvua. Maeneo
yanayopata mvua za kutosha huzalisha chakula cha kutosha pamoja na ziada. Kwa
maeneo ambayo yamezalisha ziada, wanayo fursa nzuri ya kupeleka ziada hiyo
kwenye maeneo mengine ambayo hayazalishi vizuri.
“Vilevile,
nchi yetu imezungukwa na nchi ambazo hazina fursa kubwa ya kilimo kama
tuliyonayo. Miongoni mwa nchi hizo ni kama Uganda, Kenya, Congo, Sudan na
nyinginezo. Hii ni fursa nyingine ya soko kwani tukizalisha vizuri, uhakika wa
soko la nje, ni mkubwa pia” Alikaririwa Mhe Hasunga
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amezitaja mada zitakazojadiliwa katika mkutano huo
kuwa ni pamoja na Fursa ya biashara ya mazao ya nafaka katika soko la Afrika na
uwezo wa Tanzania kuzalisha nafaka na wafanyabiashara kushiriki kikamilifu, Upotevu
wa mazao ya nafaka baada ya mavuno, mkakati wa Taifa wa kudhibiti na matokeo ya
utafiti wa hali ya maghala yalivyo hapa nchini, Uongezaji thamani katika mazao
na kuboresha mazingira ya biashara ya nafaka na Mfumo wa masoko na uzoefu.
Alisema
kuwa mada hizo zitatoa nafasi pia ya kuelewa vizuri tasnia ya nafaka ili kuwa na
maazimio ambayo yatajibu changamoto mbalimbali hususani ya upatikanaji wa taarifa
na utumiaji vizuri wa fursa zilizopo katika tasnia hiyo.
“Nitoe
rai kwa washiriki wote, tusikilize kwa makini, tuwe wawazi, na kwa uhuru tujadili
mada hizo kwa mapana na marefu, ili baada ya siku mbili hizi, tutoke na
maazimio yatakayojibu changamoto za tasnia hii ya Nafaka” Alisisitiza Mhe
Hasunga
MWISHO
No comments :
Post a Comment