Jeshi
la Polisi nchini limezuia safari za saa 24 za mabasi kwa baadhi ya
mikoa kwa sababu ya kiusalama na kuwataka wamiliki wa mabasi hayo
kuzingatia maagizo yaliyotolewa ili kulinda usalama wa wananchi.
Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 2 na Kamishina wa Oparesheni na
Mafunzo, Liberatus Sabas ambapo amesema licha ya kuruhusu mabasi yote
nchini kutembea usiku bila kulala sehemu yoyote, Jeshi la polisi
limebaini kuna baadhi ya maeneo zoezi hilo limebidi lisubiri kidogo ili
wajipange kwa ajili ya usalama na watakapojiridhisha safari hizo
zitaendelea kama kawaida.
Sabas
amesema mabasi yanayotoka Dar es Salaam kuelekea Mikoa ya Kagera,
Kigoma, Katavi hayataruhusiwa kutembea saa 24 kutokana na sababu za
kiusalama.
Kamishna
Sabas amesema zuio hilo litahusu pia mabasi yanayotoka Dar es Salaam
kuelekea wilaya mbalimbali za mkoani Tabora ambayo yatalazimika kusimama
Tabora Mjini na baadaye kuendelea na safari wilayani.
Amesema
mabasi yanayotoka mikoa ya Kagera, Katavi, Kigoma kwenda Dar es Salaam
yataruhusiwa kutembea saa 24 kama kawaida kutokana na eneo la Morogoro
na Dar es Salaam kuwa salama wakati wote.
"Mabasi
haya yalikuwa yakitoka kwenye mikoa hiyo yalikuwa yanalala Morogoro,
lakini kutokana na hali nzuri ya kiusalama yataendelea na safari hadi
Dar es Salaam," amesema Kamishna Sabas.
Amesema
mabasi yanayotoka Dar es Salaam kuelekea katika mikoa hiyo yatalazimika
kulala wilayani Kahama kisha kuendelea na safari.
No comments :
Post a Comment