
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa
Wizara ya Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar, wakati wa
kuwasilisha Utekelezaji Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018
hadi Juni 2019, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
leo,23-8-2019.(Picha na Ikulu).

WATENDAJI mbalimbali wa Idara za
Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar wakiwa katika
ukumbi wa mkutano wakati ikiwasilishwa Ripoti ya Utekelezaji wa Bajeti
na Mpango Kazi wa Wizara yao, Mkutano huo ukiongozwa na Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(Picha
na Ikulu)

WAZIRI wa Vijana Utamaduni Sanaa
na Michezo Zanzibar Mhe,. Balozi Ali Abeid Karume, akiwasilisha ripoti
ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi
Juni 2019, wakati wa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar,
kulia Naibu Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo
Zanzibar Mhe. Lulu Msham Abdalla na Mshauri wa Rais Sanaa na Utamaduni
Mhe. Chimbeni Kheri.(Picha na Ikulu).

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Vijana
Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Ndg Amour Hamil Bakari,
akiwasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi
Julai 2018 hadi Juni 2019, kushoto Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti
Bi. Saum Ali Said na Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ndg. Joseph
Kilangi.(Picha na Ikulu)

MSHAURI wa Rais Masuala ya Sanaa
na Utamaduni Mhe Chimbe Kheri akizungumza wakati wa mkutano na Uongozi
wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar, kuzungumzia
Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara hiyo uliofanyika Ikulu
Zanzibar.(Picha na Ikulu)
No comments :
Post a Comment