Rais
Magufuli amemtaka Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa
kusimamia wawekezaji wasisumbuliwe katika uwekezaji wa viwanda.
Ametoa
tamko hilo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha 21st Century Food and
Packaging, kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam, kinachomilikiwa na
mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo Dewji).
“Watendaji
ndani ya serikali pamoja na Waziri wa vianda yuko hapa, tusiwaumize
vichwa wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza katika nchi yetu, nimepata
taarifa kuna baadhi ya wawekezaji wanawekewa masharti ya ajabu na
wengine wanaombwa rushwa, sasa mnawazungusha kwanini hela ni yake
haujamsaidia yeye anakuja kuwekeza ili watu wako wapate ajira,” amesema
“Waziri
wa Biasha kama kuna watendaji wako ndani ya serikali bado hawajaona
mwelekeo wa awamu ya tano wakae pembeni sisi tuendelee kwenda mbele
kwani tunataka wawekezaji waje, akiwa na hela yake muoneshe eneo
akajenge kiwanda chake na akishamaliza serikali itakusanya kodi, Tanesco
watauza umeme, Dawasco watauza maji kwani hiyo ndiyo njia ya kuijenga
nchi,”
“Waziri
wewe ni kijana nenda ukafanye kazi kwa manufaa ya nchi, na mimi
ninawaomba mkatangaze mema ya nchi yetu kwani serukali ya Tanzania ya
awamu ya tano inapenda wawekezaji ndio maana tumefuta kodi zaidi ya 54
na sio rahisi kufanya hivyo lakini tunafanya kwa kuangali mbele,”
amesema.
No comments :
Post a Comment