*****************
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe amefanya ziara fupi kuona Mradi
mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam –
Morogoro Agosti 22, 2019.
Katika ziara hiyo Bi. Anne alipata
fursa ya kutembelea Stesheni ya reli ya kisasa inayojengwa
eneo la
Stesheni jijini Dar es salaam pamoja na kutembelea eneo la Vingunguti
kuona kipande cha reli ya kisasa kilichotandikwa eneo hilo ambapo Bi
Anne alionesha kufurashishwa na kasi ya ujenzi.
“Nimekuja kuona hatua kubwa ambayo serikali imechukua ya kujenga
reli ya kisasa ninachoweza kusema kwa niaba ya nchi ninazoziwakilisha
ni kwamba huu si mradi wa Tanzania pekee bali ni mradi wenye manufaa kwa
nchi zilizofungamana katika ukanda huu” alisema Bi. Anne
Aidha Bi. Anne ameipongeza
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutekeleza Mradi mkubwa
wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kwa kutumia mapato ya ndani pia
ameahidi kuwa Balozi kueleza yale aliyoyaona katika Mradi wa SGR
“Naipongeza serikali ya Tanzania kwa kuamua kujenga mradi huu kwa kutumia vyanzo vya ndani” Nitafikisha ujumbe huu juu ya hiki tulichokiona leo” alisema Bi. Anne’
“Naipongeza serikali ya Tanzania kwa kuamua kujenga mradi huu kwa kutumia vyanzo vya ndani” Nitafikisha ujumbe huu juu ya hiki tulichokiona leo” alisema Bi. Anne’
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema
kuwa taasisi za kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia zinaweza
kukamilishaMradi huu kwa kuufadhili siku zijazo
“Ni matumaini yangu kwamba kwa siku zijazo tutakapokuwa tunatafuta njia za kufadhili mradi huu taasisi za kimataifa ikiwemo benki ya dunia tutaweza kuja kukamilisha mradi huu” alisema Bi. Anne
“Ni matumaini yangu kwamba kwa siku zijazo tutakapokuwa tunatafuta njia za kufadhili mradi huu taasisi za kimataifa ikiwemo benki ya dunia tutaweza kuja kukamilisha mradi huu” alisema Bi. Anne
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi na
Miundombinu ya Reli Mhandisi Felix Nlalio amesema kuwa wameupokea ujio
huo kwa furaha na kwa kuwa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia amejionea
mwenyewe kasi ya ujenzi na amefurahishwa na ubora wawa kazi.
No comments :
Post a Comment