Fundi
Mchundo wa TANESCO Leah Sostheness akitoa elimu kwa wananchi
waliotembeela banda la TANESCO kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa
viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu leo
Agosti 2, 2019.
Wananchi wakipata elimu kuhusu matumizi
bora na sahihi ya umeme kutoka kwa watalamu wa TANESCO viwanja vya
Nykabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Agosti 2, 2019.
Afisa
Masoko wa TANESCO, Adelina E. Lyakurwa (wapili kulia) na na Afisa
Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Shirika hilo Mkoa wa Simiyu, Bw. Ben
Kirumbo, wakiwahudumia wananchi
Fundi Mchundo wa TANESCO Leah Sostheness, akitoa elimu kwa wanafunzi
Afisa Uhusiano TANESCO Makao Makuu, Bi. Samia Chande (kushoto), akitoa elimu kuhusu shughuli mbalimbali za TANESCO
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MAMIA
ya wananchi wakiwemo wanafunzi wa shule za sekondari Mkoani Simiyu na
mikoa jirani, wamefurika kwenye banda la Shirika la Umeme Nchini TANESCO
kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa
Bariadi Mkoani Simiyu ili kupata elimu kuhusu matumizi bora na sahihi
ya umeme.
Wananchi
hususan wanafunzi wa shule za sekondari waliweza kuuliza maswali
mbalimbali kuhusu Shirika la Umeme ikiwa ni pamoja na kazi za shirika
hilo, ambapo maafisa wa TANESCO waliokuwa kwenye banda hilo walitoa
ufafanuzi kuhusu maswali hayo ikiwa ni pamoja na kuwaeleza kuwa kazi za
TANESCO ni Kuzalisha, Kusafirisha na Kusambaza Umeme.
Pia
wananchi walipata fursa ya kujifunza matumizi sahihi ya umeme, ikiwa ni
pamoja na kuchukua tahadhari umeme unapokatika ambapo walielezwa kuwa
ni vema kuzima vifaa vyote vinavyotumia umeme pindi umeme unapokatika,
na viwashwe tu pale umeme unaporudi.
Wananchi
pia walielezwa miradi mbalimbali ya TANESCO inayotekelezwa na Shirika
hilo kwa niaba ya Serikali ambapo walielezwa miongoni mwa miradi hiyo
midogo na mikubwa ni kama ule uliozinduliwa hivi majuzi na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa ujenzi wa
mradi mkubwa wa umeme wa mto Rufiji (Bwawa la Nyerere) mkoani Pwani
ambapo utakapokamilika ujenzi wake mwaka 2022 utazalisha umeme Megawati
2115.
Maonesho
hayo ambayo yanafanyika kitaifa mkoani Simiyu yalizinduliwa Agosti 1,
2019 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan na kauli mbiu ni "Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa
Uchumi wa Nchi". Maonesho hayo yatafikia kilele Agosti 8, 2019.
No comments :
Post a Comment