
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
Mkoa wa Pwani ni
miongoni mwa mikoa nchini, yenye idadi kubwa ya wagonjwa wenye
vikope(Trachoma) huku wilaya inayoongoza ikiwa ni Mkuranga yenye
wagonjwa hao 1,041,wilaya ya Rufiji 191,Kisarawe 243 na Kibiti 207.
Hayo yalibainika katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa vikope iliyozinduliwa wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.
Mkuu wa mkoa huo,
mhandisi Evarist Ndikilo akiwa ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo
aliiasa jamii kuachana na imani potofu na badala yake wajitokeze kupima
ugonjwa huo ili kuweza kupatiwa matibabu na kuondokana na upofu .
Aidha, alitoa rai kwa viongozi wa kijamii kuwapeleka wagonjwa wenye vikope katika kambi za uchunguzi ili kupatiwa matibabu.
Nae meneja mradi wa
IMA WORLD HEALTH, Alex Msumanje akielezea magonjwa yasiyopewa kipaombele
aliyataja kuwa ni matende,mabusha,minyoo ya tumbo,kichocho,usubi na
trachoma(vikope).
Kaimu mratibu wa
magonjwa yasiyopewa kipaumbele wizara ya afya Oscar Kaitaba alisema
watu takribani 11,350 wameshafanyiwa urekebishaji wa kope katika wilaya
21.
Alifafanua, aliwaomba
wananchi kujitokeza kufanyiwa urekebishaji wa kope zao kwani huduma
hiyo ni bure na mradi huu unafanywa katika mikoa 6 ikiwemo Manyara,Lindi
,Pwani Arusha,Mtwara,na Dodoma.
Kampeni hiyo katika mkoa wa Pwani itafanyika kwenye wilaya nne ikiwa ni pamoja na Kibiti,Kisarawe,Mkuranga na Rufiji.
No comments :
Post a Comment