
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la
Arusha Sifael Kulanga akimkabidhi rasmi eneo la mradi wa ujenzi wa
barabara ya Kisongo bypass Mkandarasi wa Ujenzi wa barabara hiyo Lang
Shang ambaye ni mhandisi wa barabara wa kampuni ya Snohydro ya China kwa
ajili ya kuanza ujenzi wa barabara nje kidogo ya jiji la Arusha leo
picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Mstahiki
Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro Buhay akisikiliza taarifa kutoka
kwa kaimu mkurugenzi Sifael Kulanga wakiwa pamoja na Mhandisi wa
barabara wa Snohydro Lang Shang mara baada ya makabidhiano hayo ya
ujenzi wa barabara ya kisongo bypass nje kidogo ya jiji la Arusha picha
na Ahmed Mahmoud Arusha
Mstahiki
Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro Buhay akisikiliza taarifa kutoka
kwa kaimu mkurugenzi Sifael Kulanga wakiwa pamoja na Mhandisi wa
barabara wa Snohydro Lang Shang mara baada ya makabidhiano hayo ya
ujenzi wa barabara ya kisongo bypass nje kidogo ya jiji la Arusha picha
na Ahmed Mahmoud Arusha
Baadhi
ya Maofisa kutoka jiji la Arusha na Kampuni ya ujenzi ya Snohydro
wakifuatilia makabadhiano hayo mara baada ya kutembelea eneo la mradi wa
ujenzi wa barabara ya kisongo bypass wenye urefu wa kilimeta 3,44 picha
na Ahmed Mahmoud Arusha 
Picha ya pamoja mara baada ya
kukagua eneo la ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass itakayogharimu
kiasi cha billion 4.106 hadi kukamilika mwezi januari mwakani picha na
Ahmed Mahmoud Arusha.
*****************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Halmashauri
ya Jiji la Arusha limepata Fedha za nyongeza kiasi cha bilion 4,106 kwa
ajili ya ujezi wa barabara ya kisongo Bypass yenye urefu wa kilometa
3.44 kupitia fedha za mradi wa TSCP inayoratibiwa na benki ya dunia
chini ya Ofisi ya Raisi Tamisemi
Mradi
huo ambao tarehe 27 mwezi huu umekabidhi na Halmashauri ya Jiji la
Arusha kwa
Mkandarasi Kampuni ya Ujenzi ya Snohydro ya nchini china
utatekelezwa kwa muda wa miezi minne hadi Januari mwakani.
Akizungumza
mara baada ya kuukabidhi mradi huo kwa kampuni hiyo Kaimu Mkurugenzi wa
Jiji la Arusha Sifael Kulanga ambaye pia ni Mwanasheria wa jiji hilo
amesema kuwa mradi huo ni wanyongeza na utatekelewa ndani ya miezi
minne.
Alisema
kuwa mradi huo utasaida sana kuondoa changamoto za msongamano katikati
ya jiji la Arusha na una manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi na
utasaidia usalama kwenye uwanja mdogo wa ndege badala ya kukata katikati
ya uwanja barabara hiyo itasaidia kuchepuka pembezoni mwa uwanja.
“Barabara
hii ina umuhimu mkubwa sana katika uwanja wetu wa ndege na maeneo ya
shule ya sekondari na itafungua fursa kwa wanaowahi katikati ya jiji
kutoka stand kubwa ya mabasi ya mkoani inayotarajiwa kujengwa Olasit”
Kwa
upande wake Mhandisi wa barabara wa kampuni ya Snohydro watakaojenga
barabara hiyo Lang Yang Shang alisema kuwa wataifanya kazi hiyo ndani ya
muda uliopangwa na kwa viwango vilivyowekwa na kwa ubora.
Alisema
kuwa barabara hiyo na udogo ulipo hautawapa tabu kuikamilisha ndani ya
wakati hivyo kuweza kukamilika bila kuwepo vikwazo vyovyote hivyo kuomba
ushirikiano wakati wote wa ujenzi huo.
Awali
akitoa taarifa ya mradi huo Mhandisi Agustini Mbuya alisema kuwa
barabara hiyo ni muunganiko wa bypass na itarahisisha mchepuko na
kusaidia usalama na kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutenga
fedha hizo.
Alisema
kuwa mradi huo utaanza ujenzi rasmi tarehe 11 mwezi ujao na leo ndio
makabidhiano kwa jiji kumkabidhi rasmi mkarandari kwa ajili ya Ujenzi
huo wa barabara
Nae
Mstahiki meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro alisema kuwa Barabara
hiyo ni sehemu ya mkataba uliosainiwa wiki iliyopita na utakuwa
kielelezo cha kueleza jinsi utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa
wananchi mwaka ujao jinsi serikali ilivyotekeleza miradi.
No comments :
Post a Comment