
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru (aliyevaa shati jeupe)
akizungumza wakati wa kikao na Balozi wa Jamhuri ya Korea, Mh.
Tae-ick-Cho ambaye leo ametembelea Hospitali ya Taifa
Muhimbili-Mloganzila.

Balozi Tae-ick-Cho akizungumza jambo wakati wa kikao hicho mapema hii leo katika Hopsitali ya Mloganzila.

Baadhi ya viongozi wa
MNH-Mloganzila pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa Korea nchini,
wakimsikiliza kwa makini Balozi Tae-ick-Cho ambaye ameahidi kushirikiana
na Hospitali ya Mloganzila katika kutatua changamoto zilizopo.

Balozi Tae-ick-Cho (wa kwanza
kulia) akiwa na ujumbe wake, wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi
Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru (wa kwanza kushoto) mara baada ya
kumalizika kwa kikao, wa pili kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.

Balozi Tae-ick-Cho (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof.
Lawrence Museru (kushoto), kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji
MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.
…………………….
Balozi wa Jamhuri ya Korea
Tae-ick-Cho leo amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Hospitali
ya Taifa Muhimbili – Mloganzila na kuahidi ushirikiana katika kutatua
changamoto mbalimbali kwa lengo la kuendelea kuboresha utoaji wa huduma
za afya nchini.
Pamoja na mambo mengine katika
mazungumzo hayo Balozi Tae-ick-Cho pia amezungumzia jinsi ya kuboresha
mfumo wa TEHAMA uliokuwepo katika kusimamia utoaji wa huduma za afya
hospitalini.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema watanzania
wanapenda kuona hospitali hii ikifanya kazi iliyokusudiwa ya kutoa
huduma, elimu na utafiti na kusisitiza kuwa hilo ndio kusudio kubwa la
Rais John Magufuli.
“Lengo letu ni kuhakikisha
hospitali hii inafanya kazi kama inavyotakiwa hasa ukizingatia ni
hospitali kubwa na ya kisasa hivyo tutaendelea kuboresha huduma zetu ili
kufikia malengo yaliyokusudiwa” amesema Prof. Museru.
Balozi Tae-ick- Cho mapema hii leo amefika MNH-Mloganzila kwa lengo la kufahamiana na kuzungumza na uongozi wa hospitali.
No comments :
Post a Comment