Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Khamis Kigwangalla, ameipa siku saba Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kuhakikisha wanapeleka mapendekezo
ya namna gani watawahakikishia wawekezaji malighafi.
Katika mapendekezo hayo, amewataka kila mwaka walau kwa kipindi kisichopungua miaka mitano waweze kukopesheka kwa urahisi.
Dk. Kigwangalla amesema hayo, alipokuwa akizungumza katika mkutano wake
na wadau wa Sekta ya Misitu uliofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa, ambapo amesikiliza changamoto zinazowakabili na kuahidi
kuzifanyia kazi.
“Kuhusu suala la mikataba ya kuwazia wadau wetu vitalu, TFS ninawapa
siku saba mniletee mapendekezo ya kina ni kwa namna gani tunaweza
kuwahakikishia wadau wetu ambao ni wawekezaji kwenye viwanda kwa sababu
tuna uwezo wa kuwatambua sasa tunawezaje kuweka utaratibu ambao
utawahakikishia malighafi kila mwaka walau kwa kipindi kisichopungua
miaka mitano ili waweze kukopesheka kwa urahisi ,” amesema.
“Hili ni jambo ambalo halipaswi kushindikana hivyo mjipange mtakavyoweza
lakini mtuletee wizarani mapendekezo ni kwa namna gani mtaweka uhakika
kwa wadau wetu ambao ni wawekezaji kwenye sekta ya bidhaa ya misitu
watapa malighafi kwa uhakika walau katika kipindi cha miaka mitano,”
amesema.
Aidha amesema kuwa kwa mwaka Tanzania inaharibu misitu katika eneo la
ukubwa wa hekari laki 4.5, ambapo amewapongeza wakazi wa mikoa kusini na
baadhi ya mikoa ya Kaskazini na Kaskazini Magharibi kwa jitihada
wanazozifanya za kupanda miti kibishara kwa kusema wanasaidia katika
ikolojia ya maisha duniani,” amesema Dk. Kigwangalla.
No comments :
Post a Comment